Mwnamuziki wa Nigeria Davido ametoa shukrani kwa mke wake Chioma baada ya kumzalia mapacha.
Wanandoa hao mnamo Oktoba 9 walikaribisha watoto mapacha mvulana na msichana, mwaka mmoja baada ya kifo cha mtoto wao wa kiume Ifeanyi.
Davido anadaiwa kutumia milioni 14 kununua mikoba ya mkewe Chioma Pia amemnunulia nyumba yenye thamani ya milioni 134.
Maelezo ya zawadi za Davido kwa mkewe yamefichuliwa na mwanahabari Kemi Olunloyo ambaye alimshauri Davido kunyamaza ili kuepuka hatari zinazoweza kutokea za kiusalama.
Mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii wanasema Chioma anastahili wakati huu baraka za mapacha.
Chapisho lake la mwisho kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa mwaka mmoja uliopita alipokuwa akishiriki ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa marehemu mtoto wao.