Mkewe Njugush aonyesha wazi jumba lao lenye ghorofa mbili na magari ya kifahari

Magari mawili aina ya Range Rover nyeupe na Toyota Prado nyeusi yalikuwa yameegeshwa nje ya nyumba hiyo.

Muhtasari

• Mnamo Jumatatu, Oktoba 16, Celestine alichapisha video akionyesha maeneo ya nyumba hiyo.

• “Niliamua kukuonyesha maisha yangu na kijana mkulima. Nilipokuwa nikiolewa, sikujua alikuwa mkulima mwenye bidii,” 

Celestine Ndina akiwa kwa nyumba yake. Hisani:YouTube
Celestine Ndina akiwa kwa nyumba yake. Hisani:YouTube

Celestine Ndinda, mke wa mtumbuizaji Timothy Kimani almaarufu Njugush, ameweka wazi kwenye mitandao  picha ya nyumba yao ya kifahari.

Mnamo Jumatatu, Oktoba 16, Celestine alichapisha video akionyesha maeneo ya nyumba hiyo.

Njia ya kuendesha gari ilikuwa imepambwa maridadi meusi na mekundu maua yenye waridi yaliifanya nyumba hiyo kupendeza kweli kweli.

Magari mawili aina ya Range Rover nyeupe na Toyota Prado nyeusi yalikuwa yameegeshwa nje ya nyumba hiyo.

“Niliamua kukuonyesha maisha yangu na kijana mkulima. Nilipokuwa nikiolewa, sikujua alikuwa mkulima mwenye bidii,” alisema.

Kisha akaamua pia kuonyesha sehemu ya nyuma ya nyumba ambapo wanatumia kufanyia ukulima wa aina mbali mbali.

Pia alionyesha mbwa wanaowafuga kwa usalama, na Njugush alidokeza kuwa mfugaji wa mbwa.

Kisha Njugush alionyesha baadhi ya miti tofauti ya matunda katika boma, ikiwa ni pamoja na mapapai na maembe.

"Nimetumia nafasi iliyobaki kwa rosemary, mint na aloe vera. Unahitaji kutumia nafasi yoyote hata kama ni sehemu ndogo."

Celestine kisha alishiriki picha ya nje ya boma iliyozungukwa na miti ambayo mumewe alikuwa amepanda akisema Njugush hutumia  muda mwingi kwa ukulima.

"Yeye hutumia masaa mengi na miti yake," alisema.

Celestine hapo awali aliwapa mashabiki mtazamo wazi wa mambo ya ndani ya jumba lao la kifahari.

Mama wa watoto wawili alionyesha sebule yao kubwa na chumba cha kulia cha kupendeza chenye mapambo ya ndani.

Wanandoa hao mashuhuri walihamia kwenye jumba lao la kifahari mnamo 2019 kabla ya kukamilika.