Fimbo ya mbali haiui nyoka ni kauli ya Wema Sepetu muigizaji mashuhuri kwa waskilizaji wake katika kituo cha Radio Furaha FM nchini Tanzania.
Kulingana na Wema suala la mahusiano ya mbali kwa wachumba ni jambo ambalo halifai kwa maana mapenzi haya hayadumu kwa muda mrefu .
"Mahusiano ya mbali yanahitaji ukarimu na uaminifu wa hali ya juu ,wachumba wanafaa kuwa pamoja kila wakati ,mahusiano ya mbali yanachangia undaganyifu",alisema Wema.
Muigizaji huyu maarufu alisimulia jinsi alivyotoka kwa mahusiano alipokuwa kwenye mahusiano ya mbali baada ya kumaliza miezi miwili, akisimulia licha ya kupendana na mpenzi wake utenganisho huu uliafikiwa na wote kwa kuwa kwake ilikuwa kama kuharibiana muda.
"Nilivumilia nikachoka ,mpenzi wangu alikuwa mbali nami kila mara tuliwasiliana kwa simu, alinitumia jumbe za mapenzi lakini kwangu mapenzi haya yalinichosha nilikosa hamu na ladha ya mahusiano haya mpaka ikafikia kutengana kwetu, kwa maana nilijihisi mpekwe", alisema.
Wema alisema kwamba katika mahusiano ya mbali, wachumba wanafaa kutembeleana mara kwa mara ndiposa suala hili lisichangie kuachana kwa wachumba.