Diamond, Mbosso waeleza cheni zao zilivyokatika jukwaani na kupelekwa Uingereza kutengenezwa

Mikufu yao ya dhahabu yenye michoro ya vichwa vyao inatajwa kuwa za gharama mno.

Muhtasari

•Diamond platnumz na Mbosso wamesimulia jinsi mikufu  yao yenye vito vya dhahabu ilikatika walipokuwa wakitumbuiza wafuasi wao.

•Diamond alidokeza kuwa mkufu wake ulisafirishwa hadi Uingereza kwa kituo kimoja ili kufanyiwa ukarabati  kurudisha sehemu iliyokatika.

Mbosso na bosi wake Diamond Platnumz
Image: HISANI

Mastaa wa Bongo nchini Tanzania Diamond platnumz na Mbosso wamesimulia jinsi mikufu  yao yenye vito vya dhahabu ilikatika walipokuwa wakitumbuiza wafuasi wao.

Diamond Platnumzs kwa upande wake alisimulia,"Mkufu wangu ulikatika kipande  kimoja wakati nlipokuwa nikitubuiza wafuasi wangu kwa kuwa ni wa gharama niliweza kuagiza wenye ujuzi waniuganishie."

Msanii huyu alidokeza kuwa mkufu wake ulisafirishwa hadi Uingereza kwa kituo kimoja ili kufanyiwa ukarabati  kurudisha sehemu iliyokatika.

Nyota huyu wa Bongo alieleza kuwa mikufu yake ni ya gharama mno na kwa kawaida yeye huchagua maeneo ambayo atakayovaa wakati wa tamasha na ziara yake.

Kwa upande wa msanii Mbosso alieleza kuwa ,"Mkufu wangu wenye mchoro wa kichwa changu ambao umeundwa kwa dhahabu ulikatika ila nashukuru kwa kuwa nilitumana kwa kituo hicho hicho   Uingereza na ukarudishwa. "

Wawili hawa walisimulia  hayo walipokuwa kwenye mahojiano ya moja kwa moja ndani ya basi walimokuwa wakisafiria.

Mikufu hiyo ya  dhahabu yenye michoro ya vichwa vyao inatajwa kuwa za gharama mno. Kulingana na mmoja wa watangazaji wa wasafi media ambaye aliwahoji, zinagharimu zaidi ya millioni 45  za Kenya.