logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Prof Jay afunguka kuhusu ugonjwa wake "Nilitumia miioni 50 kwa sindano tu!"

"Nilikuwa nachoma mara 5 kwa wiki. Kwa wiki milioni 25 " alisema.

image
na Radio Jambo

Habari06 November 2023 - 09:11

Muhtasari


• Msanii huyo alimshukuru rais Samia kwa kumpigania kufanikisha kwenda kwake India kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa figo lake.

• Alisema kwamba anatamani kukutana naye ili kumpa maua yake akisema kwamba, “kitendo alichokifanya alikifanya kama mama.”

Professor Jay

Kwa mara ya kwanza tangu aliporuhusiwa kuondoka hospitalini, msanii na mwanasiasa Professor Jay amezungumza na mashabiki wake na kufunguka kwa undani kuhusu hali yake ya afya ambayo ilimlaza hospitalini kwa kipindi cha Zaidi ya mwaka mmoja.

Jay alifanya mahojiano na kituo cha redio na runinga ya Clouds ambayo alifichua kwamba alikuwa na tatizo la figo kufeli.

Kwa undani, msanii huyo alielezea makubwa na mengi ambayo aliyapitia na msaada ambao alipat kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya Tanzania.

Jay alifichua kuanzisha wakfu wa kushughulikia tatizo la figo lakini pia kutoa hamasisho kwa jamii kuhusu ugonjwa wa kufeli kwa figo.

Jay alitangaza kwamba alitumia hela ndefu sana kwa ajili ya sindano moja tu ambayo ilimpa nafuu.

“Watu wengi wanakufa sana kutokana na tatizo la figo. Ndio maana nikasema wakfu wangu uanze na suala la figo. Kuna sindano nilikuwa nachoma kwa siku milioni tano asubuhi na jioni, ile sindano ndio iliniamsha. Nilikuwa nachoma mara 5 kwa wiki. Kwa wiki milioni 25 na kila siku nilikuwa nachoma mara mbili, na nilichoma sindano 10 kwa hiyo ni milioni 50, hiyo ni sindano tu, bado kusafisha figo,” alisema.

Msanii huyo alimshukuru rais Samia kwa kumpigania kufanikisha kwenda kwake India kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa figo lake.

Alisema kwamba anatamani kukutana naye ili kumpa maua yake akisema kwamba, “kitendo alichokifanya alikifanya kama mama.”

Itakumbukwa Jay alikaa katika sadaruki kwa kipindi kirefu sana ambacho ni karibia miezi minne pasi na kuzungumza wala kumtambua mtu yeyote.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved