logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Awinja wa Papa Shirandula afichua kwa utani sababu ya makalio yake madogo

Awinja amesimulia sababu ya juu ya kuwa na makalio mdaogo kinyume na akina dada wengine..

image
na

Habari08 November 2023 - 06:30

Muhtasari


• Wakati wa mahojiano na Oga Obinna, Awinja alitania kwamba makalio yake madogo,yalisa.

• "Tulikuwa tunakalia hio engine ndio maana mimi niko na makalio madogo. Ilichomeka mtu wangu, iliiva ulikuwa unafika nyumbani haga inawaka moto,"

JACKY VIKE MAARUFU AWINJA

Mchekeshaji na Mwigizaji Jacky Vike maarufu Awinja amefunguka  na kusimulia sababu ya makalio yake kuwa madogo kinyume na akina dada wenzake kutoka Magharibi.

Wakati wa mahojiano na Oga Obinna, Awinja alitania kwamba makalio yake madogo,yalisababishwa na  jinsi alivyokuwa akisafiri hadi nyumbani kwao kijijini alipokuwa mdogo.

“Nimezaliwa Nairobi. Lakini sisi tulikuwa tunaenda kijijini  sana. Kama kila sikukuu na wakati  tukifunga  shule ikiwepo Aprili, Agosti, Desemba, sheria za baba yangu lazima tungeingia Kabiet Escort. hizi ni zile basi za kitambo kabla Ugwe, Homeboys, Eldoret Express, ile engine yake ilikuwa ndani ya basi so tulikuwa tunakalia hio engine ndio maana mimi niko na makalio madogo. Ilichomeka mtu wangu, iliiva ulikuwa unafika nyumbani haga inawaka moto,"alisema.

Kama kusisitiza , Awinja alisema kwamba siku hizo, safari zilikuwa ndefu sana.

"Siku hizo safari zilikuwa ndefu sana, fupi zaidi ilikuwa kama masaa 8. Unapoondoka saa 5 asubuhi, utafika saa 4 au 3 usiku. Mambo yamebadilika siku hizi tunasafiri kwa saa sita,” alibainisha.

Wakati huo huo alifichua ni lini mara ya mwisho alitumia usafiri wa umma hadi nyumbani kwake kijijini,akifafanua utofauti wa jinsi ya kusafiri kwenda kijijini na jinsi ya kusafiri kwenda ngambo.

“Utamu wa kwenda mashambani sidhani kama ni kwa ndege. Siwezi kwenda Ulaya kwa ndege na kisha kwenda kijijini kwenye ndege tena. Lazima kuwe na tofauti. Inabidi uende kwa basiili ufurahie mazingira. Mara ya mwisho kupanda basi ilikuwa mwaka huu. Haikuwa kuigiza, ilikuwa ni kujifurahisha tu  nikitoka nyumbani, nilikuwa na Shix(Kapienga) tulikaa nyuma. Tulirushwa tulirushwarushwa mpaka tukafika,” alisema.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved