logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Betty Kyallo asimulia changamoto za kifedha zilizomkumba baada ya kupoteza kazi ya utangazaji

Wakati huo, rafiki yake ambaye alikuwa anamdai pesa alikuwa ametishia kumtangaza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 November 2023 - 09:40

Muhtasari


  • • Akizungumza  kwenye kipindi cha Chipukeezy, Kyallo alifichua kwamba ingawa tayari alikuwa akiendesha biashara yake ya saluni, hakuwa na uhakika ikiwa ingemtosha kuendeleza majukumu yake ya kifedha.
  • • “Sikulipwa nilipoacha kazi yangu ya mwisho ya runinga, na sikujua nifanye nini, licha ya kuwa na biashara ya saluni. "
Betty Kyallo

Aliyekuwa mtangazaji Betty Kyallo ameshiriki safari yake ya kuacha kazi ya utangazajii wakati wa janga la COVID-19 na na changamoto zilizomhandama.

Akizungumza  kwenye kipindi cha Chipukeezy, mama huyo wa mtoto mmoja alifichua kwamba ingawa tayari alikuwa akiendesha biashara yake ya saluni, hakuwa na uhakika ikiwa ingemtosha kuendeleza majukumu yake ya kifedha.

“Sikulipwa nilipoacha kazi yangu ya mwisho ya runinga, na sikujua nifanye nini, licha ya kuwa na biashara ya saluni. Ilikuwa wakati wa janga la COVID-19, na sikujua jinsi ningeweza kulipa bili zangu.Si rahisi kuendesha biashara, haswa ikiwa unapaswa kulipa wafanyikazi wako kwa wakati. Kuna changamoto nyingi, na kumekuwa na wakati ambapo nimefikiria kuacha. Ushindani katika biashara ni mgumu, hasa wakati amabpo watu wengi wanafanya biashara sawia na yako."

Katika mahojiano yaliyopita, Betty alisema aliendelea kubadilisha maeneo ya biashara yake ya saluni kwa vile ilikuwa ikitatizika.

Saluni ya Betty Kyallo ‘Flair by Betty’ ilifunguliwa kwa umma mnamo Aprili 14, 2018, katika jengo la FCB Mihrab kwenye Barabara ya Lenana.Baadaye alitangaza kuhamisha biashara yake hadi eneo pana na la kifahari zaidi.

Mnamo Juni 2020, Flair By Betty ilihamia Rose Avenue na uzinduzi wake ulipambwa na Mama Ida Odinga.

“Weka mikakati tu, kisha uipe muda, usizuie mambo, haswa biashara, kwa sababu Corona iko nasi hivyo tuchukue tahadhari," Betty alisema wakati huo.

Kisha ikahamia Rose Avenue na makutano ya Barabara ya George Padmore huko Kilimani.

Betty alisema kuzindua eneo jipya ilikuwa zawadi kwake aliposherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 34.

Betty pia anajihusisha  ‘After Shave by Flair,’ Kinyozi ya hali ya juu iliyoko katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi ambayo ilizinduliwa rasmi mnamo Januari 2021.Pamoja na ile aliyozindua huko Meru mnamo Mei 2023.

Katika video ya hivi majuzi, Betty Kyallo alisimulia shinikizo za kifedha ambazo yeye, kama wengine wengi, hukabili licha ya umaarufu wake kwa  umma kama mtu mwenye mafanikio.

"Mara nyingi, maisha ni magumu. Hata nyie mkiangalia Betty anatamba na kufungua biashara baada ya nyingine na wakati mwingine mnadhani ninafanya vizuri. Mara nyingi, baadhi ya mapambano mnayopitia ni yale yale ninayopitia pia,” alisema.

Wakati huo, rafiki yake ambaye alikuwa anamdai pesa alikuwa ametishia kumtangaza kwenye mitandao ya kijamii ikiwa deni hilo halingelipwa mara moja.

"Ni sawa kuwa na deni. Mtu  ananipigia simu na kutishia kunifichua kwenye mitandao ya kijamii ikiwa sikulipa,” Kyallo alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved