logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera Sidika ndio changuo langu Kenya Harmonize asema

Harmonize asimulia hisia zake kwa mwanasosholaiti Vera Sidika.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 November 2023 - 10:35

Muhtasari


  • •Msanii huyo kwa kauli yake alimsifu Vera Sidika akisema iwapo angepata nafasi ndiye mwanadada wa Kenya ambaye siku zote angemchangua kama mpenziwe. 
Vera Sidika na Harmonize

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefunguka kwa kusema kuwa mwanasosholaiti Vera Sidika ndio mwadada  nchini Kenya anyeweza kumchumbia iwapo angeaza kuchumbiana nchini.

Msaanii huyo maarufu nchini Tanzania alisema  hayo wakati alipokuwa akitumbuiza wafuasi wake wa Kenya katika eneo moja la burudani mjini Thika.

Harmonize alifunguka hisia zake kwa Vera  Sidika wakati alipokuwa akiwasifu wanadada wa Kenya waliokuwa wakinengua viuno huku wakimshabikia alipokuwa akitumbuiza jukwaani.

"Mara kwa mara mimi hujiuliza kwanini sijawahi chumbia warembo wazuri wa Kenya,kumbe nakosa mengii aaaaah...kuna manzi mmoja wa Nairobi nammezea sana siku nitalewa nitasema ni nani ....kuna mtu ameniambia Vera Sidika hana mchumba ni kweli,"aliuliza.

Msanii huyo kwa kauli yake alimsifu Vera Sidika akisema iwapo angepata nafasi ndiye mwanadada wa Kenya ambaye siku zote angemchangua kama mpenzi wake.

Harmonize alikuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili kwa tamasha moja ambalo aliwatumbuiza wafuasi wake,huku akisema kuwa mji wa Nairobi ndio moja kati ya miji mikuu amepata nafasi ya kutumbuiza mara nyingi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved