Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu alianza wiki na povu kali kwa wakosoaji wa maumbile yake katika mitandao ya kijamii.
Kupitia uurasa wake wa Instagram, Wema Sepetu alipakia rundo la picha akionekana kulenga wakosoaji wake katika chapisho la awali kuhusu umbile la kifua chake.
Wakosoaji walikuwa wamemsuta vikali kwamba maziwa yake ‘yamelala’ na wengine hata kupendekeza kwamab ili kudumisha ulimbwende wake, afanye kama wanavyofanya warembo wengine kwa kumwaga kiasi kirefu cha hela kwa ajili ya upasuaji wa kurekebisha maumbile yao ili kudumisha urembo.
Wema akiwajibu, alianza kwa kuthibitisha kwamba ni kweli maziwa yake yamelala, akisema kwamba ni maumbile yake ha hawezi fanya chochote kuyaficha, huku pia akifichua kwamba anafahamu yamelala na hana mpango wowote wa kutafuta huduma za upasuaji kuyarudisha katika shepu na muonekano wa kisichana.
“Kwa nilivyopungua mlikuwa mnategemea nitakuwa na saa sita... Nyie kumbe wehu eeh😅😅😅 Ndio yamelala haswa ndo maumbile kwani kuna tatizo gani... Na sina mpango wa Surgery...” Wema Sepetu alisema.
Mrembo huyo aliyeshinda tuzo ya mrembo bora nchini Tanzania mwaka 2006 amekuwa akipitia changamoto mbalimbali ikiwemo kutukanwa mitandaoni kutokana na muonekano wake lakini pia kutokuwa na mtoto licha ya kukiri kwamba amefanya majaribio kadha wa kadha pasi na mafanikio.
Hivi majuzi, ameburuzana na mamake kwa kile alihisi kwamba mzazi wake anajaribu kumratibia maisha bila kuwa na ufahamu kwamba yeye ni mtu mzima sasa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi huru.
Mamake alivamia tafrija yake na mpenzi wake Whozu akiteta kwamba anasikia tu mitandaoni kwamba bintiye ana mpenzi na wanakula bata mjini lakini hajawahi hata siku moja kumtambulisha kwake, jambo lililombughudhi.
Mama mzazi pia alisema kwamba anasikitika na hali ya bintiye kwani mabinti rika zake akiwemo Jokate Mwegelo ambaye ni afisa wa huduma za kiserikali, wanafanya mambo makubwa lakini bintiye amesalia tu katika mapenzi tu, akisema kwamba bado hajajitambua na mpaka atakapojitambua, maisha yake bado yatakuwa ya kusuasua tu.