Rais William Ruto ameshidwa kuongoza nchi -Eric Omondi asema

Wakenya wamechoka na hali ya bidhaa kuogezwa bei kila siku Eric Omondi afunguka

Muhtasari

•Eric alisema kuwa visa vingi vya wakenya kujitia kitazi zimechangiwa na ugumu wa maisha ambao umechangiwa na serikali ilioko madarakani

Mchekeshaji na mwanablogu  maarufu nchini Kenya Eric Omondi amemkosoa Rais William Ruto akisema kuwa ameshidwa kuongoza nchi.

Omondi alisema kwamba ahadi nyingi ambazo rais aliahidi wakenya bado hazijatimizwa na kwamba amekuwa akifanya kinyume cha ahadi alizotoa.  

Alisema kwamba sasa ni kinaya kuwa baadhi ya hudumu za serikali ambazo zilikuwa na bure sasa zinatozwa ada. Miongoni mwa hhuduma ambazo serikali inapanga kutoza ada sasa vitambulisho vya kitaifa.

"Vitabulisho ni mojawapo ya stakabadhi muhimu kwa mkenya badala ya serikali kutoza ada ingechukua hatua ya hata  kuifanya rahisi kwa wakenya  kupata,"alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa Rais Ruto hawezi kuongoza taifa kwa maana hata baada ya muda wa mwaka mmoja na miezi saba madarakani uchumi wa nchi unaedelea kudhoofika.

"Rais ameshindwa kuendesha nchi,nina uhakika wa asilimia mia moja, kuwa rais Ruto hawezi kuongoza nchi kwa kuwa  muda amekuwa madarakani ameonyesha wazi kwa kupadisha bei za bidhaa muhimi,"alisema Eric Omondi.

Eric alisema kuwa baadhi ya visa vingi vya wakenya kujitia kitazi zimechangiwa na ugumu wa maisha ambao umechangiwa na serekali ilioko madarakani.

"Vijana wengi wamekata tamaa, ugumu wa maisha wengi hawana kazi,bei ya mafuta imekuwa ghali wengi wameshidwa na safari ya maisha ndiposa visa vya wakenya kujitoa uhai vimeongezeka,"alisema.