Mchungaji mmoja kwa jina Pasta Yohana amemkashifu vikali msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau akisema atakuwa mkosi kwa mwaka mpya 2024.
Pasta huyo alisema hayo baada ya msanii huyo wa injili Syokau kuonekana jijini Nairobi na bango lenye maadishi ya kutafuta mchumba.
"Justina alimuacha Mungu,ndio maana amepagawa na mapepo ndiposa amejitokeleza mitaani akitafuta mwanaume kwa maana mwili wake umekuwa ngome la 'shetani', kuna jambo anapanga kufanya kuaribu mwaka ujao.
"Yeye ni mchawi wa mwaka ndio maana kwenye utunzi wake wa nyimbo miaka anayoimba maisha yamekuwa magumu,yeye ni debe tupu ambalo alina maana,kelele tupu tu,"alisema mchungaji huyo.
Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu wa mitandao mchungaji huyu alisema kwamba huenda msanii Justina anajishirikisha na ulimwengu wa giza na kuna jambo amepangia kwa mwaka wa 2024 kwa kutoa kafara.
Hayo yalitokea baada ya msanii Justina Syokau kuzua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana katikati mwa jiji la Nairobi akiwa anazunguka na bango akitana mwanamume wa uchumba.
Katika bango hilo, Justina aliweka wazi kwamba kigezo cha kwanza cha mwanamume anayemtaka ni sharti awe tajiri wa kiwango cha ubilionea na pili sharti awe na miaka 25 tu.