Mchekeshaji na YouTuber, Oga Obinna kwa mara nyingine tena ameonesha nia ya kuendelea kutupa ndoana yake katika bahari ya mapenzi akiwa na matumaini ya Amber Ray kunasa kwenye chambo lake.
Mchekeshaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akionesha mapenzi yake ya dhati kwa mwanasosholaiti Amber Ray licha ya kujua fika kwamba ni mke wa mtu, alipakia picha iliyohaririwa ya jamaa anayekimbia mimba.
Katika picha hiyo, mtu alihariri mwanamume aliyevalia kanzu na kuweka kichwa chenye sura ya Oga Obinna akitoroka huku nyuma yake anaandamwa na wanawake wanne wote wajawazito.
Obinna alicheka uhariri huo na kusema kwamba aliyekuja na wazo la kumuonesha kwamba yeye anaweza kuikimbia mimba wala si kweli.
Alisema kwamba yeye hawezi kuikimbia mimba, na haswa ikitokea kwamba mimba anayozingiziwa kuwa yake inatoka kwa mwanasosholaiti Amber Ray, katu hatokimbia bali ataikubali kuiwajibikia mia kwa mia.
“Haki mnikome, mimi siwezi kimbia Amber Ray ama mimba,” Obinna alisema kwa emoji za kucheka.
Obinna amekuwa akimfuata Amber Ray kwa mbinu zote, akionekana kuwa mtu wa kwanza kushambikia matatizo katika uhusiano wa mwanasosholaiti huyo na mumewe Kennedy Rapudo.
Obinna alisifia kuvunjika kwa uhusiano wao akisema kwamba angalau sasa anaweza pata nafasi ya kukubaliwa na Ray kuwa mpenzi wake, japo alikiri kwamba bado hajapata gari aina ya Range Rover ambalo Ray aliweka wazi kuwa mwanamume yeyote anayetaka kuwa mpenzi wake hicho ndicho kigezo cha kwanza cha kumchuja.