Jamaa mmoja anayetania kuwa ni mpenzi wa zamani wa msanii Zuchu amejitokeza na kumuandikia msanii huo ujumbe wenye aya ndefu akimtaka warudiane.
Hii ni baada ya msanii Diamond Platnumz kudai hadharani mbele ya kadamnasi ya wafuasi Zaidi ya milioni 16 kwenye Instagram yake kwamba yuko single wala hana mpenzi tena – akionekana kumpiga chini Zuchu ambaye kwa muda wamekuwa wakionekana kama wapenzi.
Kwa ujumbe ambao jamaa huyo kwa jina Clam Cris aliandika kwenye Instagram, moja kwa moja aliashiria kwamba wamewahi kuwa kwenye mapenzi na Zuchu lakini uhaba wa hela ukasababisha kuvunjika kwa penzi lao.
Mchekeshaji huyo alisema kwamba kwa vile sasa ameshapata hela jinsi Zuchu alimuasa wakati wa kuachana, ni vizuri waweze kurudiana, akisema kwamba hajawahi mpenda mwanamke mwingine jinsi alivyokuwa anampenda mrembo huyo hitmaker wa Sukari.
“Wewe ndiye uliyenifanya nipigane kwa uchungu ili yale yaliyopita yasijirudie 😢 Kila nikikumbuka siku uliniambia kuwa pesa ni ya thamani sana katika maisha yetu Bindam kwa sababu watu huacha vitu wanavyovipenda kwa sababu ya pesa, lakini ni ngumu kuacha pesa kwa sababu ya vitu wanavyovipenda,” mchekeshaji huyo aliandika.
“Sijawahi kupenda kama jinsi nlivyo kupenda zuhura.Wewe ndiye uliyenifundisha maana ya mapenzi zuhura licha ya yote karibu tena kwenye maisha yangu ❤️” aliongeza.
Alhamisi, Mitandao ya kijamii ilishika moto kufuatia taarifa za Diamond kukana kuwepo na mpenzi yeyote na kuvutia maoni kinzani.
Kukana kwa Diamond kulikuja siku chache baada ya mamake kufanya mahojiano na kusema halitambui penzi la mwanawe na Zuchu.
Haat hivyo, saa chache baadae, Diamond alirudi kwenye mitandao ya kijamii na kutengua kauli yake ya awali.
Alisisitiza kwamba yeye bado yuko kwenye mapenzi na Zuchu wala hakuna kitakachowatenganisha, akiashiria kwamba watu walimnukuu vibaya katika kauli yake ya awali kuwa yuko single.