Msanii wa singeli, Dulla Makabila kutoka ameamua kuachia wimbo wa kumchamba aliyekuwa mpenzi wake, muigizaji Zaylissa siku moja baada ya kuvishwa pete ya uchumba na mwanamume mpya, Haji Manara.
Makabila ambao walikuwa kwenye huba zito na mrembo huyo kabla ya kutimukia kwa Manara ambaye amekuwa na mazoea ya kuoa na kuacha, amempiga uppercut muigizaji huyo kwa kudai kwamba muda wote walikuwa pamoja, Zaylissa alikuwa mbovu sana katika kupika.
Makabila katika diss track hiyo anamchamba Zaylissa kwa uduni wake katika masuala ya jikoni na kumuasa kwamba ni muda sasa ajitahidi ili Haji Manara – ambaye ni albino – asijue kwamba hajui kupika. Amemtaja Haji kwenye wimbo kama ‘Mzungu’.
Wimbo ulitoka saa chache tu baada ya Zaylissa na Manara kusimamisha mji usiku wa kuamkia Ijumaa kwa tukio lao kubwa la kuvishana pete.
Wimbo huo unakwenda kwa jina Furahi na ndani mle Makabila amefunguka mambo mengi haswa akirejelea penzi lake na Zaylissa lakini pia akimshambulia kwa vijembe vya aina yake.
“Najua ulinipenda, ulimbukeni wa umaarufu ndio sababu ukaniacha, ukimcheki Wolper na Uwoya, upon a tamthilia ya kazi inakuchelewesha. Kumbuka ile siku nilitaka penzi ukanikazia kisa laki 8, name sikukukatalia ukasema nitume kwanza ndio mzuka nitakugea…” sehemu ya wimbo huo unaimba.
“Yaani tupo ndani ya ndoa, lakini bado ulinidangi, name sishangai njaa ndio inavyokuwa. Umeniacha mimi mzungu amekuvutia, mpende baba wa watu, ana ugonjwa wa kuzimia. Ukileta manjege utapewa kesi ya kuua,” aliendelea.
Kwenye kiitikio, Makabila anaimba;
“Wewe furahi tu nimekuacha furahi, umepata mzungu furahi. Mimi si ulininywea P2, basi huyo mzungu ndio umzalie. Na ile siri yetu hadi leo nimeificha, na wewe jitahidi mzungu asijue kuwa hujui kupika.”
Kwenye vesi nyingine pia aliwaponda wasanii ambao walishangilia ndoa ya Manara na aliyekuwa mkewe, akisema kwamba ni wanafiki kwani walifanya vivyo hivyo wakati yeye na Zaylissa wanafunga ndoa.