Mkuza maudhui chipukizi, Dem wa FB amewazuzua wengi baada ya kudai kwamba ndio mara ya kwanza kuvaa vazi la thamani Zaidi wakati wa kuhudhuria hafla ya siku ya kuzaliwa ya mwanawe Kennedy Rapudo na Amber Ray.
Katika sherehe hiyo iliyofurikwa mastaa mbalimbali kutoka kwa sekta ya Sanaa na burudani, kuadhimisha mwaka mmoja wa kuzaliwa kwa Afrikanah, Dem wa FB nimiongoni mwa watu waliovutia Zaidi na vazi la rangi nyekundu.
Akizungumza na waandishi wa habari za burudani, Dem wa FB alisema kwa kutania kwamba hajawahi ng’ara jinsi alivyong’ara katika siku hiyo maalum, akitania kuwa alitaka kupendeza Zaidi ili kumvutia ‘crush’ wake, Kennedy Rapudo.
Mchekeshaji huyo alisema kwamba kwa Obinna show Live huwa anaenda kama amevaa mavazi ya kuuzwa katika soko la tambarare la Gikomba lakini katika hafla hiyo, alijikakamua na kuvaa vazi la Zaidi ya elfu 15 pesa za Kenya.
“Sijawahi ng’ara hivi, kwa Obinna huwa naenda vile niko. Nguo hii ilinigharimu 15k, nimeng’ara hivi kwa sababu ya crush [Rapudo], kwa Obinna huwa naenda na nguo za Gikomba. Make-up nimelipa 7k, nywele nikasuka na 4k, kucha nikawekewa na 3k na viatu nimenunua 4k,” Dem wa FB alisema huku akisisitiza kwamba gharama yote ni bei ya shamba mahali.
Dem wa FB alisema kwamba hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na Kennedy Rapudo ana kwa ana, kwani mara nyingi huwa wanazungumza kupitia kwa simu.
Pia alimpa maua Amber Ray, akisema kuwa yeye ndiye alimsaidia kumrembesha kwa mavazi na vipodozi, pamoja na msaidizi wake.