logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rapudo akiri kutokuwa na tatizo mkewe kufanya sajari kuongeza maziwa, aahidi kulipia gharama

"Nitakachotaka kujua ni gharama tu na nitatoa pesa ili aende kufanikisha sajari ya maziwa yake,” Rapudo alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani20 May 2024 - 12:04

Muhtasari


  • • Alisema kwamba kwa mwanamume yeyote ili kupendwa na mwanamke mrembo kama Amber Ray, mwanzo sharti uwe na Imani kwake kwani ni mtu mzima anayejua anachotaka katika maisha.
Kennedy Rapudo na mkewe Amber Ray

Mfanyibiashara Kennedy Rapudo amefunguka kwamba hana tatizo na mkewe, Amber Ray kufanya sajari ya kuongeza ukubwa wa maziwa yake.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani, Rapudo alisema kwamba yeye haoni tatizo kwa mkewe kufanya sajari yoyote ya kuongeza urembo wake, kwani yeye [Rapudo] ana pesa za kutosha kugharamia kitu chochote cha kumpendezesha mkewe.

Alisema kwamba ikiwa Amber Ray atahitaji kuongeza urembo kwa kufanya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa maziwa yake, yeye yuko radhi kugharamia utaratibu huo wote, mradi tu aorodheshewe bajeti.

“Mke wangu ana uwezo na uhuru wa kufanya chochote anachotaka kufanya kwa sababu ana uungwaji mkono wangu. Hata kama ni kutaka kuwa na maziwa makubwa, mradi tu ana furaha na hilo. Nitakachotaka kujua ni gharama tu na nitatoa pesa ili aende kufanikisha sajari ya maziwa yake,” Rapudo alisema.

Mfanyibiashara huyo ambaye walikuwa wanasherehekea mwaka mmoja tangu kupata mwanao wa kwanza pamoja, Afrikanah, alisema kwamba anafahamu fika kuwa mapenzi ya Amber Ray kwake ni ya kuigiza bali ni ya kweli.

Alisema kwamba kwa mwanamume yeyote ili kupendwa na mwanamke mrembo kama Amber Ray, mwanzo sharti uwe na Imani kwake kwani ni mtu mzima anayejua anachotaka katika maisha.

“Mke wangu ananipenda kwa sababu nimemruhusu kufanya chochote anachotaka kufanya na kuwa yeyote anayetaka kuwa. Kwa mtu yeyote kuchumbiana na mwanamke mrembo, ni sharti uwe na Imani naye kwa sababu ni yeye ni mtu mzima anayejua anachotaka katika maisha,” Rapudo alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved