logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Ng’ang’a asikitishwa na mzozo wa ardhi baina yake na serikali

Mumekuja kupiga magoti hapa sasa leo umekua mkubwa, unataka kumchallenge Mungu wangu?

image
na Davis Ojiambo

Burudani30 May 2024 - 08:52

Muhtasari


  • •Namshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru. Hata kama mulisema ni mlevi heri Uhuru mara mia moja. Nipeleke kule mtanipeleka. 
  • •Sasa leo hii nyinyi wakubwa muskie hii si kanisa na mulikuwa hii kanisa ikiweko sasa leo mnavote No

Mwazilishi wa Neno Evangelist Mchungaji Ng’ang’a alionekana kukejeli serikali ya Kenya kwanza na utawala wake hii ni kufuatia mzozo wa ardhi ambapo kanisa lake limejegwa.

Akihutubia waumini wake katika kanisa lake, Ng'ang'a alishiriki kusikitishwa kwake na serikali ya Kenya Kwanza, haswa uongozi , akisema alipendelea Rais wa zamani Uhuru Kenyatta  kwa sababu serikali haijatetea ardhi yake kunyakuliwa.

“Namshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru. Hata kama mulisema ni mlevi heri Uhuru mara mia moja. Nipeleke kule mtanipeleka. Kiwanja hii ilipoanza kuchukuliwa, Uhuru aliposkia alipiga simu moja tu.

Sonko aliwahi pigia Uhuru simu akamwambia hii ni kanisa sasa wanasema barabara inapitia tangu siku hiyo, kesi iliisha. Rais Ng’ang’a alisema.

Anaendelea kusema jinsi alivyosikitishwa na serikali ya Kenya Kwanza na wanasiasa ambao sasa wanapiga kura dhidi ya uwepo wa kanisa lake, akiongeza kuwa ikiwa ndivyo wanavyotaka, basi atalazimika kwa furaha.

“Sasa leo hii nyinyi wakubwa muskie hii si kanisa na mulikuwa hili kanisa ikiweko… sasa leo mnavote No…basi muvote kesho mje mchukue mimi sina shida nitaenda tu mbinguni nikiwa uchi.” Mchungaji Ng’ang’a alishiriki.

Aliukubali utawala wa Rais Uhuru Kenyatta kwa sababu alitetea ardhi ya kanisa lake kila mara, na kwa hilo, huwa anashukuru ikilinganishwa na serikali ya sasa, ambayo inataka kutumia ardhi hiyo.

“Uhuru aliposkia hii kiwanja ina shida, alipiga simu tuu ilikua ikatwe hapo mbele sijui ina nini niliona wakiongea nikaona wamechukua vitu vyao hawakurudi leo hii mko wakubwa. hii si klabu ni nyumba ya mungu!” PST. Ng’ang’a alisema.

Alimalizia kwa kuhutubia Serikali , wanaotaka kutumia ardhi la kanisa, kwamba wakifanya wanavyotaka, basi watakabiliwa na ghadhabu ya Mungu.

“Mumekuja kupiga magoti hapa sasa leo umekua mkubwa, unataka kumchallenge Mungu wangu? Ngoja uone naapa mbele za Mungu mtaona." PST. Ng’ang’a alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved