Mwanamuziki na pia mwanasiasia Kevin Bahati na mwimbaji Stivo Simple Boy wamewafurahisha watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kubadilishana mazungumzo wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Bahati kjwenye Netflix.
Simple Boy alikuwa mmoja kati ya wasanii waliohudhuria sherehe hio ya uzinduzi.
Hitmaker huyo wa kibao 'Mihadarati' ndio aliwasisimua wengi kwa mavazi alliyovalia.
Msanii huyo alivaa suruali ya maroon na kuifananisha na koti la rangi ya dhahabu ambalo lilikuwa na alama za maroon kwenye kingo.
Pia alivalia shati la cream na viatu vyeusi, hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa mastaa wa kiume waliovalia vizuri kwenye hafla hiyo.
Alikuwa na muda wa mazungumzo na Bahati, ambaye hakuweza kuacha kupongeza muonekano wake huku akimsifu kwa ufundi wake.
"Nimeona amejivika sura ya muuaji. Uko sawa sana, unafanya vizuri. Na nimefurahi.
Hata msimu wa pili, njoo tufanye shoo, kwa Empire ya Bahati." Bahati alisema.
Kisha wakabadilishana namba za simu huku watu wakimpongeza Simple Boy kwa mwonekano wake.