Dadake Diana Bahati, Val, amefunguka kuhusu jinsi anavyokabiliana na unyanyasaji mtandaoni.
Akishiriki katika mahojiano, alisema yeye hajishughulishi na wakosoaji, kwani akifanya vile ni kuwapa nafasi ya kuendelea kuzua matatizo, na badala yake anachagua kuwapuuza.
“Siwashughulikii. Siwazii kamwe juu yao, hawako kwenye shughuli yangu kamwe. Namaanisha, sijali watu wanasema nini." Val alisema.
Val alifafanua kuwa shoo The Bahati's Empire haijaandikwa, kwani ni onyesho halisi linaloakisi kile kinachotokea katika maisha halisi.
“Haijaandikwa Kwanza kabisa, mimi na kiherehere, tuko pamoja, kwa hivyo haijaandikwa.
Ni halisi sana, na huo ndio utu wangu, wenye watanipenda watanipenda.
Unachokiona ndicho kinachotokea, sio kweli na imeandikwa hakuna mahali unaambiwa aty, sema hivi, sema hivi." Aliongezea.
Alifunguka kuhusu sifa za mwanamume anayemtaka, akisema lazima mtu huyo awe na uwezo wa kifedha na awe na sifa sawa na za mume wa dadake, Kevin Bahati.
"Ikiwa una pesa, kwanza kabisa, wacha niseme kwamba huyu ndiye mwanaume wa aina yangu, sio kimwili.
Ningetaka mwanaume ambaye ana sifa sawa na Bahati, kwa sababu Bahati ni mbunifu.
Ningependa mtu ambaye ana nguvu za kifedha na kiakili. kihisia-moyo, kiroho katika kila nyanja, pili, mtu anayetanguliza mahitaji yangu, na tatu, mtu anayemcha Mungu.” Val alisema.