logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dj shiti afunguka kuhusu changamoto alizopitia akianza ucheshi

DJ Shiti alisema kuwa alianza kwa kuhama kutoka nyumbani kwake Nakuru hadi Nairobi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani12 June 2024 - 13:51

Muhtasari


  • • DJ Shiti alisema kuwa alianza kwa kuhama kutoka nyumbani kwake Nakuru hadi Nairobi kwa sababu alitaka kupata changamto mpya.
  • •Pia alisema kuwa alifikiria kujaribu kitu tofauti na alichokuwa akifanya ili asiwachoshe mashabiki wake.
92568426_231459261546688_5080697964784774052_n

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Steve, anayefahamika kwa jina la uigizaji DJ Shiti, amefichua changamoto .

Akizungumza katika kipindi cha Mic Check Podcast, DJ Shiti alisema kuwa alianza kwa kuhama kutoka nyumbani kwake Nakuru hadi Nairobi kwa sababu alitaka kupata changamto mpya.

Alieleza ukumbi wa michezo waliyokuwa wakitumia ulikuwa mdogo, na wakati wao, ili msanii akuchague, ulihitaji kuwa katika jiji ambapo fursa zilikuwa mingi.

“Kujaribu usanii tuh unajua lazima ugrow. Theatre ilikua ndogo. Saa hii vile online imekuja ndio unaeza fanya usanii popote pale.

Lakini kitambo ni lazima ukuje Nairobi ndio umake it saa hii kuna wasee wanafanya usanii from anywhere…so mchezo ulibadilika.” Dj Shiti alisema:.

Pia alisema kuwa alifikiria kujaribu kitu tofauti na alichokuwa akifanya ili asiwachoshe mashabiki wake.

“Na mimi sipendi sana kufanya kitu kimoja for long na nataka nikifanya hii kitu naenda kwa ingine.

kwa sababu akili ya binadamu imeumbwa kwa kuchoka na kitu moja.” DJ Shiti alieleza.

Akizungumzia jinsi alivyotulia, DJ Shiti alikiri kuwa haikuwa rahisi kwa sababu hata ndugu zake wa karibu ambao alidhani wangemsaidia walimgeuka. Na akaishia kukosa makazi mjini.

Safari ya Dj Shiti kutua jijini haikuwa rahisi kwa sababu baada ya kufanya kazi  na kulipwa, bado alikuwa akihangaika kubaki jijini.

Na hio ilimpelekea yeye kupatana na mtu asiye mjua ambaye alimhakikishia kuwa atampeleka mahali pa kulala usiku huo.

Kwa mshangao, mtu huyo ambaye hakujulikana jina lake alimpeleka tu Mathare na kumwacha amekwama huko.

“Nilienda Ngara kutafuta mahali pa kulala nikameet boy fulani akaniambia nakupeleka mahali udoz but usitoke nje…Akaniitisha dooh yangu akitisha Kenya Cane na chipo.

After hapo akanichukua hadi mathare kufika huko akaniambia acha tupite hapa nibuy weed akabuy alafu akarukia hiyo side na kuniwacha hapo.” Dj Shiti Amesimulia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved