Mimi ni kipofu lakini nitatokea kwa maandamano ya kupinga mswada wa fedha – Robert Kigame

Kigame alisema kuwa kinachompa msukumo Zaidi wa kutaka kujiunga kwenye maandamano hayo ni kipengele ambacho kinalenga kuweka ushuru kwa viti vya magurudumu.

Muhtasari

• Baadhi ya maeneo ambayo yanashuhudia maandamano wakati huu ni Nairobi, Nyeri, Nakuru, Kisii, Eldoret miongoni mwa maeneo mengine.

Image: X

Mwinjilisti na mwanasiasa Robert Kigame amefichua kwamba atakuwepo kujiunga na vijana kwenye maandamano ya kupinga kupitishwa kuwa sheria mswada wa fedha wa 2024 jijini Nairobi.

Maandamanao hayo ya vijana yanatarajiwa kuendelea Alhamisi katika miji mbalimbali nchini Kenya, wananchi wakilenga kushinikiza wabunge kutoupitisha mswada huo ambao wanautaja kuwa vpengee vyake vinalenga kuwanyofoa kiuchumi.

Kigame, ambaye alilenga kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa 2022 bila mafanikio baada ya ombi lake kutupwa nje dakika za mwisho na tume ya uchaguzi na mipaka, EACC alisema kuwa hali yake ya kuwa mlemavu wa macho haitamzuia kutojitokeza kwenye maandamano.

Kigame alisema kuwa kinachompa msukumo Zaidi wa kutaka kujiunga kwenye maandamano hayo ni kipengele ambacho kinalenga kuweka ushuru katika uagizwaji wa magurudumu ambayo hutengenezwa nje ya nchi.

Kigame alisema kuwa kama mtetezi wa walemavu, hawezi kubali kuona viti vya magurudumu kwa walemavu kutozwa ushuru kwani hatua hii itapandisha gharama ya viti hivyo ambavyo huwasaidia walevamu kujisogeza kutoka sehemu moja hadi nyingine.

“Jamani, mimi ni kipofu, lakini nitakuwa mitaani kurudisha nchi yangu. Sitaruhusu viti vya magurudumu kutozwa ushuru.#RejectFinanceBill,” Kagame alisema.

Hata hivyo, baadhi ya watu katika mtandao wa X alikochapisha ujumbe huo walimsimi kughairi uamuzi huo kwani huenda ataathirika kutokana na vitoza machozi kutoka kwa polisi lakini akasisitiza kwamba sharti akuwepo.

Mpaka wakati wa kuchapishwa kwa Makala haya, tayari picha kutoka maeneo mbalimbali zilionyesha hali ya makumi ya vijana mitaani wakiandamana kwa Amani.

Baadhi ya maeneo ambayo yanashuhudia maandamano wakati huu ni Nairobi, Nyeri, Nakuru, Kisii, Eldoret miongoni mwa maeneo mengine.