Sababu ya Juliani kuwataka vijana kubeba Bluetooth Speaker wakati wa maandamano

Alhamisi, ripoti hiyo inapangwa kujadiliwa kwa kina na kupigiwa kura ya ndio au la, na vijana wengi wameandaa maandamano ambayo huenda yatakuwa makubwa Zaidi kufanyika bila kuongozwa na mwanasiasa yeyote.

Muhtasari

• Juliani kupitia ukurasa wake wa X, alithibitisha kwamba atakuwepo na kuwataka vijana kando na kujihami na maji, simu zao na hanchifu kwa ajili ya kufuta machozi na jasho, pia wabebe vifaa vya muziki.

Juliani
Juliani
Image: Insgaram

Rapa na mwanaharakati Juliani ameonyesha nia ya kujiunga na mamia ya vijana wa Gen Z Alhamisi mchana jijini Nairobi katika maandamano yanayoratibiwa kufanyika kwa siku ya pili wiki hii kushinikiza bunge kutupilia mbali mswada wa fedha wa 2024.

Maandamano ya kwanza yalifanyika Jumanne wakati ripoti ya mswada huo ilikuwa inafikishwa bungeni kwa mara ya kwanza na mwenyekiti wa kamati ya mipango ya fedha, mbunge wa Molo Kimani Kuria.

Alhamisi, ripoti hiyo inapangwa kujadiliwa kwa kina na kupigiwa kura ya ndio au la, na vijana wengi wameandaa maandamano ambayo huenda yatakuwa makubwa Zaidi kufanyika bila kuongozwa na mwanasiasa yeyote.

Juliani kupitia ukurasa wake wa X, alithibitisha kwamba atakuwepo na kuwataka vijana kando na kujihami na maji, simu zao na hanchifu kwa ajili ya kufuta machozi na jasho, pia aliwataka kujitokeza kwa wingi na vifaa vya muziki kama vile Spika za Bluetooth.

Msanii huyo maarufu kwa nyimbo za kiharakati alisema kwamba maandamano yao yanafaa kuchukua taswira ya tafrija na wala si kuharibu mali ya watu, akisema kuwa muziki utachangia pakubwa katika uwapa waandamaji nguvu ya kuzidi kushikiza Zaidi, wakilenga kukita kambi nje ya majengo ya vunge la kitaifa wakati mswada huo utakuwa unapigiwa kura.

“Tahadhari: Vipi kuhusu sherehe kamili kesho. Watu wabebe Bluetooth speaker.  Tunakubali playlist ya kucheza. (ngoma yoyote inaeza wapa watu motisha na nguvu) Kaende kaende!” Juliani alisema.

Kampeni ya kuunganisha vijana mtandaoni kwa ajili ya kushinikiza kuangushwa kwa mswada wa fedha wa 2024 imeshika kasi haswa katika mtandao wa X ambako wanatumia alama za reli #RejectFinanceBill2024 na #OccupyParliament.