Mchungaji Ng’ang’a ahidi kushiriki maandamano siku ya Jumanne

"Hata mimi nitakuwa kwa hiyo maandamano sasa mje na teargas mnipige,ninaweza zungumza kama mwananachi nitaacha pastor hapa wacha mtaniona tu."

Muhtasari

•Alieleza kukerwa kwake na kifo kilichotokea wakati wa maandamano wiki iliyopita na kusema wanaosababisha waendelee lakini wajue kuwa kesi yao inawasubiri na ipo siku wataondoka.

•Mchungaji Nganga alisema kuwa atakuwa katika maandamano hayo kama mwananchi wa kawaida

Nganga
Image: HISANI

Mwasilishi wa kanisa ya Neno Evangelist Mchungaji Ng’ang’a sasa amewahakikishia umma kwamba hawatatembea peke yao siku ya Jumanne, ambayo itakuwa tarehe ambapo maandamano ya pili yatafanywa kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Mchungaji Ng’ang’a, ambaye alikuwa akizungumza na waumini wake kanisani, alisema kwamba atashiriki maandamano ya nchi nzima kwa sababu ya uchovu wa serikali ya sasa ya Kenya.

Alieleza kukerwa kwake na kifo kilichotokea wakati wa maandamano wiki iliyopita na kusema wanaosababisha waendelee lakini wajue kuwa kesi yao inawasubiri na ipo siku wataondoka.

Mchungaji Nganga alisema kuwa atakuwa katika maandamano hayo kama mwananchi wa kawaida.

"Hata mimi nitakuwa kwa hiyo maandamano sasa mje na teargas mnipige,ninaweza zungumza  kama mwananachi nitaacha pastor hapa wacha mtaniona tuh." Mchungaji Ng’ang’a alisema.

Mchungaji Ng’ang’a alishiriki masikitiko yake na Serikali ya Kenya Kwanza kwa kulenga ardhi yake kila mara, ambayo anadai haifai kupokonywa kutoka kwake.

“Kuna shamba yangu iko kule naivasha acre kumi na tano naskia kuna watu wa serikali wameweka fence wamechukua acre sijui acre tano na 5,000 na moja ni yangu hapo ole wako wewe.

Siku moja mtaondoka watu wenye mashamba ndio wananyayasa wale hawana nafikiri hiyo maaandamano ingine hata mimi nitakuako,” alisema.

Hii si mara yake ya kwanza kukashifu kuhusu ardhi ya kanisa lake kwamba aliarifiwa kwamba inapaswa kuhamishwa kwa sababu iko kando ya barabara.