Bosi wa Mavin Records Don Jazzy, 41, afunguka kwanini hajaoa

Mwaka 2022, Don Jazzy alidaiwa kuwa miongoni mwa watu waliokereka baada ya msanii Rihanna kuweka wazi kwamba alikuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake ASAP Rocky.

Muhtasari

• "Mara tu unapofungua ukurasa wowote wa warembo kwenye instagram kitu cha kwanza utaona ni "unafuatiwa na don jazzy". Mwanaume huyo yuko kila mahali 😂,” aliandika.

Mtayarishaji maarufu wa muziki, Don Jazzy, hatimaye amefichua kwa nini hajaoa, huku akimjibu mwanamtandao ambaye aligundua kuwa anafuatilia kwa bidii watu kadhaa kwenye Instagram.

Itakumbukwa kuwa bosi huyo wa Mavin Records aliwahi kuoa kabla ya ndoa yake kugonga mwamba.

Mwanamtandao mmoja alienda kwenye Twitter kushiriki maoni yake kuhusu Don Jazzy.

Mwanamtandao huyo anayejulikana kwa jina la @UGBEDE__ alitoa maoni kwamba kila anapofungua ukurasa wowote wa Instagram wa mrembo, mtu mashuhuri wa kwanza kuona akimfuata mwanamitindo huyo atakuwa Don Jazzy.

"Mara tu unapofungua ukurasa wowote wa warembo kwenye instagram kitu cha kwanza utaona ni "unafuatiwa na don jazzy". Mwanaume huyo yuko kila mahali 😂,” aliandika.

Don Jazzy alikubali hili, na alikiri kwamba anapenda wanawake, na hiyo inaelezea kwa nini bado hajaoa tena.

“Mimi napenda mabinti wazuri na ndio maana sijawahi tulia kwenye ndoa,” Don Jazzy alijibu.

Mwaka 2022, Don Jazzy alidaiwa kuwa miongoni mwa watu waliokereka baada ya msanii Rihanna kuweka wazi kwamba alikuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake ASAP Rocky.

Inadaiwa kwamba Jazzy alikuwa kwa muda mrefu akimfuatilia Rihanna kwa lengo la kumuoa.