Kwa nini Nanny Rosie hatorudi tena Lebabon baada ya kurudi nyumbani Kenya

Baada ya kufika kwa wanawe, Rosie alifanya video ya wanawe wkimshukuru bosi wake wa Lebanon kwa kumruhusu mama yao kurudi kwao.

Muhtasari

• Baada ya kufika kwa wanawe, Rosie alifanya video ya wanawe wkimshukuru bosi wake wa Lebanon kwa kumruhusu mama yao kurudi kwao.

ROSIE
ROSIE

Nanny Rosie, mfanyikazi wa ndani kutoka Kenya nchini Lebanon aliyegonga vichwa vya habari mwaka jana baada ya video ikionyesha watoto wa bosi wake wakilia wakati wa kumpa kwaheri katika uwanja wa ndege alipokuwa akirudi nyumbani amerejea kwenye vichwa vya habari tena.

Safari hii, Rosie amerudi nyumbani Kenya kabisa na hatorudi Lebanon kuendelea na kazi ya ndani tena.

Licha ya kurudi Kenya mwaka jana, alikaa kwa muda na familia yake kisha kurudi Lebanon tena, hata baada ya kujizolea umaarufu humu nchini na kutunukiwa na watu mbalimbali kwa wema wake uliodhihirika na jinsi watoto wa bosi wake walivyokuwa wakimlilia kurudi.

Safari hii baada ya kurudi Kenya, Rosie ameweka wazi kwamba hatorudi Lebanon tena kwani amerudi kwa familia yake milele.

Hii ni baada ya baadhi ya watu kuzua uvumi ainati, wengine wakisema huenda amefukuzwa kazi, jambo ambalo limemfanya yeye pamoja na bosi wake kufunguka kwa nini anarudi kwa familia yake kabisa.

"Rosie aliniomba nimpeleke nyumbani, na moja kwa moja nilimkatia tiketi kama nilivyomwambia hapo awali, yeye ni mgeni kwetu. Aliwakumbuka watoto wake na akaenda tu nyumbani milele usituhukumu, na unaweza kumuuliza mwenyewe, harudi tena, kwa hivyo hakuna shinikizo," alisema bosi wake.

Baada ya kufika kwa wanawe, Rosie alifanya video ya wanawe wkimshukuru bosi wake wa Lebanon kwa kumruhusu mama yao kurudi kwao.

"Halo Mariya, asante kwa kumruhusu mama yetu arudi salama. Asante kwa zawadi ulizotutumia na kutupenda kama familia. Tunathamini kile ambacho umetufanyia na Mungu akubariki sana," alisema.

Video nyingine ilinasa kwaheri ya kihisia kati ya Rosie na watoto aliokuwa amewalea. Watoto hao walionekana wakilia sana huku wakimkumbatia Rosie kwa nguvu, wakijitahidi kumwachia.