Ezekiel Mutua alaani vitisho kutoka kwa wahuni wanaodai kuwa Gen Z

"Lakini mtu huyo alitangulia kushiriki nambari yangu hadharani na ujumbe wa uchochezi "tumsalimie" alisema.

Muhtasari

•Mutua alieleza kuwa watu hao waliotekeleza vitendo hivyo walikuwa wakifanya hivyo kwa kutozingatia kabisa maadili na ukiukaji wa haki za kimsingi za binadamu.

•Mutua alisisitiza umuhimu wa kudumisha uadilifu na heshima katika aina zote za mawasiliano, akitaja kuwa baadhi ya watu akiwemo yeye ni wa muhimu sana kutopewa vitisho.

Ezekiel Mutua
Ezekiel Mutua
Image: Facebook

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK) Ezekiel Mutua, amekashifu vikali tukio la hivi majuzi la uvamizi na vitisho vilivyoelekezwa kwake na mtu anayedai kuwakilisha Gen Z.

Katika taarifa yake aliyoweka kwenye akaunti yake ya X, Mutua alielezea wasiwasi wake kuhusu kutishiwa kwa kusema mawazo na maoni  yake.

Mutua anasema kuwa mtu, aliyejifanya kuwa mwanachama wa Gen Z, alijihusisha na kushiriki mawasiliano yake ya kibinafsi mtandaoni na kutoa vitisho kwake.

“Mmoja wa watu waliojifanya Gen Z alinitisha  kwa sababu ya maoni wangu wa awali nikisema kwamba tusichukue uhuru tunaofurahia nchini Kenya kuwa kirahisi.

Hayo yalikuwa maoni yangu na nina haki kwa hilo,” Mutua alibainisha.

Mkuu huyo wa MCSK aliangazia athari za hatari za vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wahuni, akiongeza kuwa vitendo kama hivyo ni vya nyuma na vimepitwa na wakati.

"Lakini mtu huyo alitangulia kushiriki nambari yangu hadharani na ujumbe wa uchochezi "tumsalimie" ninaweza kuthibitisha kuwa ni nambari yangu.

 Nimekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 20. Sasa itumie kama unavyotaka. Vitisho kama hivyo vya "kusalimia watu" ni vya kizamani na vya zamani," Mutua alisema.

Aidha Mutua alieleza kuwa watu hao waliotekeleza vitendo hivyo walikuwa wakifanya hivyo kwa kutozingatia kabisa maadili na ukiukaji wa haki za kimsingi za binadamu.

Mutua alisisitiza umuhimu wa kudumisha uadilifu na heshima katika aina zote za mawasiliano, akitaja kuwa baadhi ya watu akiwemo yeye ni wa muhimu sana kutopewa vitisho.

“Unawezaje kutetea Kenya bora wakati unatishia watu na kuingilia mambo yao kibinafsi? Baadhi yetu tunashikilia misingi ya juu sana ya maadili ili kutishiwa na walaghai,” Mutua aliongeza.

Tukio hilo linajiri siku chache baada ya Mutua kushauri Gen Z kuzingatia sheria na kuepuka vurugu, akisema kuwa ghasia huwanyang'anya vijana mamlaka yao.

Aliongeza kuwa vijana wanaweza tu kuwa na nguvu kwa kutenda kisheria.

"Una nguvu wakati unatenda kulingana na sheria wakati uko nje ya kabila na zaidi ya kununuliwa. Una nguvu unapochoma dhamiri zetu kwa ujasiri wako kamili, ujasiri na akili."

"Kudhulumu wengine, kunasababisha ghasia na vurugu sio nguvu."

Inakunyang’anya mamlaka,” Mutua alisema.

Zaidi ya hayo, Mutua aliwataka vijana wa Kenya wanaoandamana kutochukua hatua kinyume na Katiba, ili wasipoteze uhalali wao.