Shakib: “Gari la kwanza kumiliki ni BMW mwaka 2015, sijawahi kuchukua gari kutoka kwa Zari”

" Acha nikuambie, mimi nilimiliki gari aina ya BMW. Hilo lilikuwa gari langu la kwanza mwaka 2015. Sijui kwa pesa za Uganda ni shilingi ngapi lakini kwa Afrika Kusini ilikuwa Rand 20k,” Shakib alisema.

Muhtasari

• Wakati uo huo, mjasiriamali huyo wa mavazi ya wanaume alikanusha madai kwamba huwa anapatiwa magari ya kutembelea na Zari.

SHAKIB LUTAAYA CHAM
SHAKIB LUTAAYA CHAM
Image: INSTAGRAM

Shakib Cham Lutaaya, mumewe mwanasosholaiti Zari Hassan amefichua kwamba hakuna siku amewahi kuchukua au kupewa gari na Zari kwa ajili ya matumizi yake.

Licha ya wengi kudai kwamba ‘amewekwa’ na tajiri huyo mama wa watoto 5 mwenye makazi na biashara zake nyingi nchini Afrika Kusini, Shakib amefunguka kuwa pia ni mkwasi wa kipekee kwani alimiliki gari lake la kwanza mwaka 2015, kabla hata hawajajuana na Zari.

Katika mazungumzo na kipekee aliyokuwa akihojiwa kuhusu maisha yake na wanahabari za burudani kweney chaneli yake ya YouTube, Shakib alisema kwamba alinunua gari aina ya BMW mwaka 2015 akiwa nchini Afrika Kusini.

“Watu wanasema eti nilikuwa naazima gari, mtu unaweza azima gari na ukae nalo kwa miaka 10? Niambie mtu mmoja ambaye amewahi fanya hivyo. Acha nikuambie, mimi nilimiliki gari aina ya BMW. Hilo lilikuwa gari langu la kwanza mwaka 2015. Sijui kwa pesa za Uganda ni shilingi ngapi lakini kwa Afrika Kusini ilikuwa Rand 20k,” Shakib alisema.

Wakati uo huo, mjasiriamali huyo wa mavazi ya wanaume alikanusha madai kwamba huwa anapatiwa magari ya kutembelea na Zari, akisema kwamba tangu 2015 amemiliki magari mengi ya kifahari mengine hata amesahau.

“Kwangu mimi wakati naona mtu anasifia gari ni jambo dogo sana. Kwa sababu wakati unafanya kazi kila kitu huwa rahisi, mmekuwa mkisikia watu ambao nilikuwa nakaa nao, halafu mnategemea mimi niwe nikifanya nini wakati huo wote?...”

“…kwangu mimi gari ni kitu kidogo sana, nimemiliki magari sijui mangapi, na mimi sijawahi chukua gari lolote la Zari,” aliongeza.