Mwanzilishi wa Neno Evangelism Mchungaji James Ng'ang'a amewapongeza vijana wa Generation Z kwa kuonyesha ufupi wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Kizazi cha Gen Z hivi majuzi waliongoza maandamano ya kihistoria nchini, ambayo yalimfanya Rais William Ruto kuondoa Mswada wa Fedha wa 2024.
Akizungumza wakati wa mahubiri katika kanisa lake, Mchungaji Nga'ang'a alisifu kizazi cha Gen Z na kudai kuwa Mungu ndiye aliyewaleta ili kumlinda dhidi ya wanyakuzi wa ardhi yake.
Alisema iwapo mtu yeyote atamgusa, Gen Zs atamlinda.
"Kuna mtu alidai kuwa ardhi hii ni ya mama yake. Lakini maasi ya Gen Z yameibuka.
Mungu ameleta Gen Z wanisaidie. Wametumwa na Mungu. Wapigieni makofi. Ukinigusa, Gen Zs watakuwa hapa kesho," Ng'ang'a alisema.
Mchungaji James Ng'ang'a wa Neno Evangelism alikipongeza kizazi cha Gen Z kwa ushujaa wao kufuatia maandamano ya hivi majuzi ya kupinga muswada wa fedha.
Mchungaji Ng’ang’a hivi majuzi ameonekana kukejeli serikali ya Kenya kwanza na utawala wake hii ni kufuatia mzozo wa ardhi ambapo kanisa lake limejegwa.
Akihutubia waumini wake katika kanisa lake, Ng'ang'a alishiriki kusikitishwa kwake na serikali ya Kenya Kwanza, haswa uongozi , akisema alipendelea Rais wa zamani Uhuru Kenyatta kwa sababu serikali haijatetea ardhi yake kunyakuliwa.
“Namshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru. Hata kama mulisema ni mlevi heri Uhuru mara mia moja. Nipeleke kule mtanipeleka. Kiwanja hii ilipoanza kuchukuliwa, Uhuru aliposkia alipiga simu moja tu." alisema