Khalif Kairo aeleza sababu ya wakenya kutoandamana leo

"Usiende kwa maandamano haifai Kama unaipenda nchi yako, toa suluhisho.” Khalif Kairo alisema.

Muhtasari

•Kairo anaamini kuwa malengo yaliyokuwa yakiwafanya watu kuandamana yameshughulikiwa ambayo ni Mswada wa Fedha na mawaziri ambao wamefukuzwa kazi na aliwataka wananchi kujaribu kutumia mbinu tofauti na kuona jinsi inavyofanyika.

•Alipendekeza suluhu pekee ni kusubiri uchaguzi ujao ili kuchagua viongozi bora.

khalif Kairo
Image: Instragram

Mjasiriamali wa Kenya Khalif Kairo amefichua sababu kwa nini watu wasiandamane leo.

Kairo anaamini kuwa malengo yaliyokuwa yakiwafanya watu kuandamana yameshughulikiwa ambayo ni Mswada wa Fedha na mawaziri ambao wamefukuzwa kazi na aliwataka wananchi kujaribu kutumia mbinu tofauti na kuona jinsi inavyofanyika.

“Saa hii kwenda kwa maandamano tunaiweka nchi katika hatari ya machafuko na uchumi katika mitaa mingi, Usiende kwa maandamano haifai Kama unaipenda nchi yako, toa suluhisho .” Khalif Kairo alisema.

Kairo pia aliwakumbusha watu kuwa waangalifu na kuwafikiria wale ambao hawajalindwa na polisi pamoja na wale ambao biashara zao zinaweza kuvunjwa na pia wale wanaweza kupoteza maisha kwa jina la 'maandamano ya amani'.

Khalif Kairo, anaamini kuwa ni haki pia kuwajali wengine na pia Serikali ya Kenya isimamie kujaribu kuona kama kutakuwa na mabadiliko kwa sababu tayari walitoa hoja yao kwa kuandamana.

 Na pia maandamano hayo walionyesha Serikali kwamba watu hawakupendezwa na namna inavyotawala hasa kutoza ushuru mkubwa ambao rais alikataa kupitisha kuwa sheria.

Khalif alipuuzilia mbali ajenda ambayo watu wanatetea ambayo ni #Ruto Must Go akisema hata kama Ruto angejiuzulu bado hakutakuwa na mabadiliko kwa sababu nchi iko kwenye mzozo mkubwa.

Alipendekeza suluhu pekee ni kusubiri uchaguzi ujao ili kuchagua viongozi bora.