DJ Crème de la Crème adai ni yeye alitengeneza beat ya wimbo ‘Anguka Nayo’ miaka 7 iliyopita

Na kama hiyo haijatosha, mcheza santuri Crème de la Crème sasa ameibuka na kudai kwamba mdundo ambao umetumika katika wimbo huo ni kazi ya mikono yake ambayo ilifanyika miaka 7 iliyopita.

Muhtasari

• “Nilitengeneza Mdundo wa Anguka Nayo / Kufa Juu mwaka wa 2017 , na Tuliachia " Kufa Juu " Ft Tribeless & The Kansol , Mejja & Madtraxx Huge Huge Banger Hadi Sasa.”

DJ CREME DE LA CREME
DJ CREME DE LA CREME
Image: INSTAGRAM

Mcheza santuri Crème De La Crème ameibuka na madai kwamba ni yeye mwanzilishi na muasisi wa mdundo wa wimbo ambao umekuwa maarufu ndani ya kipindi kifupi – Anguka Nayo.

Wimbo huo ambao umepata mafanikio ya kufikisha watazamaji zaidi ya milioni moja ndani ya siku nane tu ulitolewa na kundi la vijana wanaojiita Wadagliz, wiki mbili zilizopita.

Baada ya kuachiliwa, wengi katika mitandao ya kijamii haswa katika jukwaa la X waliukumbatia wakiuhusisha na maandamano ya vijana wa Gen Z ambao wamekuwa wakimshinikiza rais ‘kuanguka’ na baadhi ya vitu kama kufutilia mbali mswada wa fedha, kuvunja baraza lake la mawaziri miongoni mwa hatua zingine.

Na kama hiyo haijatosha, mcheza santuri Crème de la Crème sasa ameibuka na kudai kwamba mdundo ambao umetumika katika wimbo huo ni kazi ya mikono yake ambayo ilifanyika miaka 7 iliyopita.

“Nilitengeneza Mdundo wa Anguka Nayo / Kufa Juu mwaka wa 2017 , na Tuliachia " Kufa Juu " Ft Tribeless & The Kansol , Mejja & Madtraxx Huge Huge Banger Hadi Sasa.”

“Songa Mbele Miaka 7 Baadaye na Hapa Tupo .. Anguka Nayo , Kuchukua Ulimwengu 💯🔥 Jiji moja kwa Wakati. Wakati mwingine ninahisi kama ninakataa lakini ni wakati wa Kunyenyekea maishani mwangu,” alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, katika chapisho hilo, aliwatambua vijana Wadagliz na kuwapa maua yao kwa kupeleka mdundo wa Kenya kimataifa na utunzi wao kwenye wimbo huo.

“Kuona Sauti ya Kenya ikivuka mipaka na kuvunja rekodi , na kuingia kwenye Hollywood 🔥 Inashangaza Tu. Nuff Heavy Love to the Young kings @wadagliz_ke .. Ni Wakati Wako. Tumeunda Wimbo wa 🔥🔥 Kenya kwa Ulimwengu 🇰🇪. @ericmusyoka Ulitenda haki kwenye Mastering na Keys za ziada 🔥 Tutasimulia hadithi hiyo,” alisema.