Mchekeshaji David Oyando, almaarufu Mulamwah, na mpenzi wake Ruth Kirui, almaarufu Ruth K,wametangaza kuwa watafichua sura ya mwanao,Oyando Junior Jumamosi hii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Mulamwah aliwakikishia wafuasi wake kuwa ataonyesha sura ya mtoto wake anayefahamika kama Oyando Junior jumamosi hii mwendo wa saa nne asubuhi.
Miezi michache iliyopita ,Mulamwah aligonga vichwa vya habari kwa mbinu yake isiyo ya kawaida ya kufichua sura ya mwanawe, Oyando Junior. Mulamwah alifichua kwamba yeye pamoja na 'bestie' wake, Ruth K, wanafikiria kufunua uso wa mtoto wao kwa njia ya kipekee.
Mulamwah alidai kuwa angetoza Ksh.100 milioni kwa wale watakaotaka kuona sura ya mwanao ,hii ni baada ya makubaliano na 'bestie' wake, Ruth K.
Mulamwah na mwenzi wake Ruth K walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Februari 10, 2024.
Wakati wa kuzaliwa kwa Oyando Junior,Mulamwah alielezea furaha yake;
"Mungu ni mkubwa, hatimaye kijana wetu yuko hapa, mrithi yuko hapa, mfalme yuko hapa. Karibu duniani mwanangu, ni hisia nzuri zaidi ulimwenguni hatimaye kukuona na kukushikilia. cant wait for us to grow & make kumbukumbu pamoja," alisema.
Kwa upande wake Ruth K alisema ;
"Tangu nilipokushika mikononi mwangu kwa mara ya kwanza, nilijua tu kuwa wewe ndiye fumbo lililokosekana maishani mwangu, vidole vyako vidogo vilivyozunguka kwenye yangu, pumzi yako na jinsi unavyonitazama kwa macho yako yasiyo na hatia. subiri kutengeneza kumbukumbu zaidi na wewe na uangalie unakua mtu wa ajabu unapendwa sana mtoto Kalamwa," Ruth K alisema.