Marapa Femi One na Khaligraph Jones wamewaacha mashabiki wao katika mtandao wa Instagram na maswali mengi baada ya kutaniana kuhusu kuwa washirika wa kundi la itikadi kali za kidini, iluminati.
Khaligraph Jones alichapisha video akiwa kwenye rafu yenye kofi nyingi huku akitangaza moja ya chapa ambazo yeye ni balozi wa mauzo.
Femi One alifika na kumtania kwa maoni kwamba rafu hiyo yenye kofia nyingi si ya mtu wa kawaida, akisema kuwa haikosi Jones ni mshirika wa iluminati.
Jones kwa upande wake alimjibu kwa utani akimshukuru kwa kumuingiza katika iluminati.
“Hiyo closet 🔥🔥 wee Uko Illuminati,” Femi One alimwaambia.
“@femi_one Asante kwa kuniingiza illuminati Femi, Wamenisaidia sana,” Papa Jones alimjibu kwa njia ya utani.
Kwa muda mrefu, kumekuwa na mjadala pevu kuhusu uhalisia wa iluminati, baadhi wakishikilia kwamba hizo ni hekaya tu za Abunuwasi na sufuria zake, wengine wakisema ni jumuiya ya kusaidia watu na wengine wakiijua kama jumuiya yenye itikadi hasi ambazo huhitaji washirika wake kutoa kafara za damu ya binadamu.
Na hili lilitdhihirika kwenye pande wa waliochangia maoni katika majibizano hayo ya utani;
“Iluminati kweli iko?” lekker 10fficial aliuliza.
“Tunapigia debe vitu vya kishetani, kweli?” inginareza John alisikitika.
“I see , hayiaa basi Jones tunaitaji House tour kama mafans” g.desay alisema.
“@khaligraph_jones inalipa😂😂” warcarpol alimuuliza.
“Hii ndo masaa ya kuitwa devil worshipper yaani unimaginable success❤️❤️omollooooooooo🔥” herlifa connections alisema.