'Muziki unalipa' - Mwanamuziki Zuchu awapa moyo wasanii chipukizi

"Mimi siendi kwenye show yoyote chini ya Tsh.20M"

Muhtasari

•Zuchu aliwahimiza wasanii chipukizi kutokufa moyo na kudai kuwa muziki unalipa kwa kiasi cha hali ya juu.

•Msanii huyo alidai  pesa kiasi ambayo alipokezwa mwaka huu ni Tsh.15M  (zaidi ya Ksh.720,000)

Zuchu
Zuchu
Image: Insta

Staa wa bongo fleva Zuchu amewahimiza wasanii chipukizi kutovunjika moyo kwa kudai kuwa muziki unalipa.

Msanii huyo mrembo kutoka Tanzani alisema kuwa wanamuziki chipukizi hawafai kukata tamaa hata kidogo.

"Tusidanganyane muziki unalipa...."

Hata  hivyo msanii huyo alifichua kiwango chake cha malipo akidai kuwa;

"Mimi siendi kwenye show yoyote chini ya Tsh.20 M, (Zaidi ya Ksh.960K),"

Vile vile aliendelea kwa kusema kuwa malipo ambayo amepokea ya chini kabisa ilikuwa Tsh.15M ambayo ni takriban zaidi ya Ksh.720,000.

"Mwaka huu show ambayo nimeifanya kwa kima cha chini nililipwa Tsh.15M (Zaidi ya Ksh.720,000) na bosi aliombwa sana hadi akasema  tuwasaidie hao ndugu zetu." Zuchu alidai.

Miezi michache iliyopita Zuchu alifungiwa kufanya show nchini zanzibar  na baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na utamaduni Zanzibar (BASSFU) kwa kumchukulia hatua mwimbaji huyo kwa muda wa miezi sita.

Kwa mujibu wa BASSFU, uchunguzi uliofanyika ulionyesha kuwa utendaji kazi wa Zuchu hauendani na mila na desturi za Zanzibar.

Hata hivyo msanii huyo,aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Alifafanua kuwa vitendo vyake vilikusudiwa kuwaburudisha mashabiki wake na akajutia athari yoyote mbaya ambayo inaweza kuwa nayo kwa jamii.

“Napenda kutumia fursa hii kuwapa pole kwa maneno niliyoyatumia katika wimbo huo uliozua tafrani katika tamasha la Full Moon Party Kendwa Beach Zanzibar hivi karibuni, najua maneno hayo yameleta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi jamii na mashabiki wangu," alisema.