Vita vya maneno vimekuwa vikitamba baina ya msanii Otile Brown na Bien kwenye mitandao ya kijamii.
Bien alimshtumu Otile Brown kwa kukosoa wimbo wake mpya aliomshirikisha Prince Indah na Adenkule.
" Otile hakuna pesa uko nayo ...unaongea kama nani?Alitoa Album haikuenda mbali...." Bien alisema.
Hata hivyo Otile Brown hakusita hata kidogo,na kupitia katika ukurasa wake wa Instagram alidai kuwa hawezi bishana na watu wanaodhani wimbo wowote maarufu ni wimbo mzur(anarejelea wimbo wake Bien)
"Siwezi kubishana na watu wanaodhani wimbo wowote maarufu ni wimbo mzuri na hivyo ndivyo mlivyoharibu mchezo.sasa mnatakiwakutingisha makalio yenu kwenye mitandao ya kijamii kusukuma bidhaa ambayo itaisha tu kwa wiki moja au mbili..." Maandishi yalisomeka kwenye ukurasa wa Insta story wake Otile.
Otile alidai kuwa yeye anaimba muziki wa asili huku akimponza Bien kwa kusema kuwa alipoteza uhalisia na hivo anaimba muziki ambao watu wanataka.
"...wewe unafanya muziki kwa kundi dogo la watu wa mjini wanaojiona kuwa wanajua maisha sana."
Aliongeza kwa kusema kuwa Bien aangazie wimbo wake wa mwisho ulio'hit na wake.Otile alidai kuwa yupo juu na hivo hajaringa wala kwenda kwenye mitandao ya kijamii kushangilia.
"Angalia wimbo wako wa mwisho uliohit na uangalie wangu ,bado ni hit kubwa zaidi nchini kwa upande wa maoni .Bado ni video ya muziki boran zaidi nchini,kwa karib mwaka na sikuhitaji kutingisha kiuno changu kwenye mitandao ya kijamii ,hizi hit mnazosema mko nazo ni gani hizo za maoni milioni 3,milioni 5? Nikifanya hit ni sahihi kabisa na siyo vitu vya kulazimisha unavyoshinda mitandao ya kijamii..."
Je,Unahisi ni nani mkali wao kati ya Bien na Otile Brown ?