Msanii na mzalishaji wa muziki,Magix Enga amefunguka kuhusu kuporomoka kwake huku baadhi ya wasanii wakijitenga kando na yeye.
Kwenye mazungumzo katika show ya ogaobinna ,Magix alidai kuwa ukurasa wake wa Facebook uliha'ckiwa.
"Kitu kilifanya Magix Empire ifail ,page yangu ya FB ili-hackiwa na ili-con wasee wengi sana.So,wasee wengi walikuwa wanadhani ni mimi na pia ma-stress zikaanzia hapo," Magix alisema.
Hata hivyo,mzalishaji huyo wa nyimbo alidai kuwa alijaribu kwa kila namna na hatimaye akafaulu kurejesha akaunti yake japo aliripoti kwa DCI ila yote iliambulia patupu na hajawahi pata msaada.
"Nilienda hadi kwa DCI Kasarani kureport na kuwaonyesha hadi contacts za watu walikuwa wamekoniwa but nothing happened so nilikufa moyo," alidai.
Aliendelea kwa kusema kuwa wasanii wengi walijitenga mbali na yeye na hakuna yeyote aliyeonyesha nia ya kumsaidia.
"Hakuna wasnii walikuja kunisaidia.Nawaonaga tu waki-like mapicha nikiteseka na nikijaribu but bado nipo.Willy M Tuva tu ndo alicome akanisaidia ndo atleast nikafanya video moja quality na yeye siyo msanii."
Magix hata hivyo kabla ya kuanza kwa mahojiano alidai kuwa bado anatumia pombe kama njia mojawapo ya kukumbana na stress.
Wiki chache zilizopita, Enga, ambaye aliokolewa awali kutoka maisha ya mihangaiko na kupelekwa katika kituo cha kurekebisha tabia na baadae kutafutiwa ajira ya kuzalisha miziki katika studio moja mjini Eldoret amekuwa akikiri katika machapisho yake hivi majuzi kwamba amerejelea katika uraibu huo.
“So sad sijui watu but wananijua sana because of my music so I drink every day because I love my fans and am always too good to everyone which I find it crazy kuongea na mtu anakujua na mimi simjui,” Magix Enga alisema.