Steve ambaye anajulikana kama Leksharaa kwenye mitandao ya kijamii amethibitisha kwa mara nyingine kuwa kuchumbiana si kwa wale walio na roho nyepesi.
Maudhui yake Steve kwenye mitandao ya kijamii huhusisha kutoa ushauri wa uhusiano wa mapenzi wenye utata.
Lekshara alionyesha kujawa na hisia za uchungu baada ya mmoja wa mpenzi wake wa zamani kumwacha na hatimaye akatua kwa mwanamke mwingine.
Kulingana naye, mwanamke aliye na 'vibe' zaidi alizungumza na mpenzi wake akimshawishi aachane naye - jambo ambalo hajawahi kufikiria lingempata.
Hata hivyo pamoja na mapenzi na mapenzi yote aliyokuwa amemwonyesha mpenzi wake, bado alimchagua mwanamke mwingine badala yake.
Vile vile aliongeza akidai kuwa alikuwa aki'simp vibaya sana hasa baada ya kuhamia jijini Nairobi.
"In my new days in Nairobi,nilkuwa simp mkubwa sana...nikanunua kakiti kadogo ka plastick niwe nakaa nje ya nyumba kutafuta network ndo nichat na huyu dem..lakini wapi..." Leksharaa alisema.
Aliongeza;
"Eiii niliona dust vibaya sana..huwa nakaa chini najiuliza maswali mengi sana...."
Lekshara anaendelea kujikusanyia wafuasi wengi na maudhui yake yenye utata ambayo watu wengi wanaonekana kuhusiana nayo.
Tazama video hapa;