logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakenya wafurahia kuona bintiye Serena Williams na bangili ya bendera ya Kenya

Baadhi ya mashabiki mtandaoni wameonyesha kufurahia

image
na Davis Ojiambo

Burudani31 July 2024 - 09:27

Muhtasari


  • •Wakenya tofauti akiwemo afisa mkuu mtendaji wa bodi ya utalii ya Kenya (KTB), June Chepkemei walionyesha kufurahia.
  • •Michezo ya Olimpiki kule Paris bado inazidi kupamba moto na kuwavutia mashabiki mbali mbali kutoka sehemu tofauti za dunia.
familia ya serena Williams

Alexis Olympia Ohanian, bintiye nguli wa tenisi Serena Williams, amezua msisimko mtandaoni baada ya kuonekana akiwa amevalia bangili ya bendera ya Kenya.

Olympia, ambaye yuko Paris kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya majira ya joto na wazazi wake Alex Ohanian na Serena,  walionekana wakitembea kwenye zulia jekundu.

Mtoto  huyo wa miaka 6 amekuwa akikusanya zawadi, ikiwa ni pamoja na 'baji' na pini kutoka nchi mbalimbali.

Hata hivyo babake Alexis, alielezea kupitia ukurasa wa X almaarufu twitter sehemu alikotoa bangili hio. 

"Kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Kenya! Alifurahi sana kukutana nao na kuwauliza pini yao (na wakampa toleo jipya zaidi kwa bangili hiyo!)," alichapisha kwenye X.

Hili lilizua hisia kutoka kwa wazawa wengi wa kidijitali, akiwemo afisa mkuu mtendaji wa bodi ya utalii ya Kenya (KTB), June Chepkemei.

"Kenya is indeed Magical," June Chepkemei alichapisha kwenye mtandao wa X.

Haya hapa ni baadhi ya maoni mtandaoni;

@footsoldierRow  - Nimefurahi kuona mtoto wa @serenawilliams akicheza bangili ya bendera ya Kenya.

@reubenmuhindi  - Ni bangili nzuri. Ningependekeza sana likizo nchini Kenya na kufurahia mambo yote mazuri ambayo nchi inapaswa kutoa. Serena na Olympia watapenda! - 

@farhiyaabass -"Mrembo kweli kweli..Angependa Kuwa Kenya. Mlete kwa ziara! "

@Nakeel - Serena anadaiwa safari ya kwenda Kenya. Muulize kuhusu hisani yake nchini Kenya ambapo alianzisha maabara ya kompyuta kwa shule ya upili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved