Mwimbaji mashuhuri wa HipHop, Cardi B, ametangaza kuwa yeye ni mjamzito huku akitarajia mtoto wake wa tatu.
Cardi B aliwafahamisha mashabaiki baada ya kuwaonyesha picha za mavazi mekundu yanayonyeshea mimba yake kwenye mitandao ya kijamii.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 31 alishiriki habari hii muda mfupi baada ya kufungua kesi ya talaka dhidi ya aliyekuwa mume wake rapa wa Migos, Offset.
Mwakilishi wa Cardi B alithibitisha kwa wanahabari husika kuwa aliwasilisha kesi ya talaka kwa kusema, "Hii haitegemei tukio lolote maalum, imekuwa ikipangwa kwa muda mrefu."
Alifungua kesi ya talaka dhidi ya Offset mnamo Jumatano, kama ilivyoripotiwa na Entertainment Tonight.
Katika chapisho lake, Cardi B, jina lake halisi ni Belcalis Marlenis Cephus, alimshukuru mtoto wake kwa kumsaidia kupitia wakati mgumu, akisema:
"Ni rahisi zaidi kuwa na mabadiliko ya maisha, mikakati na majaribu, lakini wewe, kaka yako na dada yako mmekuwa mkionyesha kwa nini inafaa kupambana!"
"Kwa kila mwisho kuna mwanzo mpya! Nimejaa shukrani kwa kushiriki msimu huu pamoja nawe, umeleta upendo zaidi, maisha zaidi na zaidi ya yote umerejesha nguvu yangu," aliandika kwenye maelezo.
Wapenzi hao wa nyimbo za hip-hop walifunga ndoa mnamo mwaka 2017 na wana watoto wawili.
Offset,kwa jina lake halisi Kiari Kendrell Cephus, pia ana watoto watatu kutoka kwa mahusiano ya awali, kulingana na Entertainment Tonight.
Katika moja ya matangazo ya moja kwa moja kwenye Instagram mnamo Desemba, Cardi B alifunua kuwa alikuwa hana mtu nayo hali hiyo ilikuwa ya muda tu.
Cardi B na Offset wamekuwa na matukio kadhaa ya juu na chini katika uhusiano wao, huku Cardi B akifungua kesi ya talaka mara mbili hapo awali.
Mashabiki walianza kudhani kuwa uhusiano wao uko kwenye hali mbaya mwishoni mwa mwaka jana wakati kila rapa aliacha kumfuata mwingine kwenye Instagram, kwa mujibu wa Entertainment Tonight.