Kwa nini Pasta Size 8 anahisi ndoa ni kama biashara

Kuingia mguu mmojà ndani ya ndoa na mwingine nje kisa unataka kuwa safe ndicho kitu kinavunja mahusiano mengi," alisema.

Muhtasari

• Utaingia mguu mmoja kwa 50% halafu ukuje kusema hakuna mwanamke amewahi kupenda kumbe wewe ndio hukuingia ndani 100%." - Size 8.

Mwimbaji huyo amezindua kanisa lake.
Size 8 na mume wake DJ Mo Mwimbaji huyo amezindua kanisa lake.
Image: MpASHO

Siku chache baada ya kutangaza kuanza safari ya maisha bila mume, mchungaji Size 8 sasa abadai ndoa ni kama biashara.

Akizungumza na mtengeneza maudhui Oga Obinna kwenye kipindi chake katika mtandao wa YouTube, Size aliwashauri watu kutoweka vikwazo wakati wanataka kuingia kwenye ndoa.

Size 8 aliwashauri watu kama wanafanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa, wasikuwe na atiati ya mguu mmoja ndani na mwingine nje, bali waingie kwa asilimia 100.

"Kuingia mguu mmojà ndani ya ndoa na mwingine nje kisa unataka kuwa safe ndicho kitu kinavunja mahusiano mengi," alisema.

"Ukiingia kwa ndoa na mguu mmoja hivyo, hutawahi patiwa 100% na yeyote juu wewe uko ndani mguu mmoja. Hivyo kwa nini utake 100% hali ya kuwa wewe uko ndani na mguu mmoja?" Size 8 alihoji zaidi.

Alisema kuwa ndoa ni kama biashara, mtu unaingia mazima bila kujali yatakayotokea mbele, iwe faida au hasara, japo wengi huingia na imani ya kupata faida.

"Utaingia mguu mmoja kwa 50% halafu ukuje kusema hakuna mwanamke amewahi kupenda kumbe wewe ndio hukuingia ndani 100%."

"Si ni kama biashara? Ndoa ni kama biashara, unaingia ikiingiana poa sawa. Kuchumbiana unaingia 100%, huwezi fanya biashara 50-50. Ikikataa ku'work unasonga kwa biashara nyingine, huwezi ingia kwa biashara kwa asilimia 50-50. Ni jambo sawia na uhusiano," aliongeza.

Japo mama huyo wa watoto wawili alitangaza kuachana na mpenzi wake Dj Mo na kufikisha kikomo cha mahusiano yao ya zaidi ya miaka 10, bado wengi wanahisi ni Kiki tu wala hawajaamini.