logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rick Ross achukua mtandaoni kulalamika rafiki anayeishi naye kwake kulala hadi 11:30am

"Huwezi kuwa unalala kwa mtu mwenye pesa. Itamuumiza mtu mmoja tu,” alihitimisha Rick Ross.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 August 2024 - 10:48

Muhtasari


  • • Alianza kwa kuwashauri wafuasi wake umuhimu wa kuanza siku alfajiri mapema kabla ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa bado anang’orota kitandani majira ya saa tano.
RICK ROSS

Msanii wa Marekani Rick Ross amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha video akilalamika vikali kuhusu hulka isiyo ya kupendeza ya rafiki yake ambaye anaishi kaitka jumba lake la kifahari.

Katika video hiyo, Rossey – kama anavyojiita kwa madoidoi, alionyesha kuchukuzwa na tabia ya mmoja wa marafiki zake ambaye anaishi naye kaitka jumba lake la kifahari kulala hadi saa tano na nusu mchana.

Alianza kwa kuwashauri wafuasi wake umuhimu wa kuanza siku alfajiri mapema kabla ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa bado anang’orota kitandani majira ya saa tano.

“Unaona ninazungumza kuhusu kulala hadi kuchelewa. Niligundua kuwa nilikuwa na mtu chini ya paa moja na mimi, na ni 11:30am? Bado amelala. Hilo haliwezi kuvumiliwa. Lazima nifanye jambo kuhusu hilo, uko tayari? Njoo nami," Ross alisema kwenye hadithi ya Instagram.

Baada ya kuingia chumbani, rafiki yake mwingine alimletea kipeperushi cha majani na kumpulizia rafiki yake aliyekuwa amelala usoni. Maskini jamaa yule aligutuka kutoka usingizini aliwa amechanganyikiwa huku Rossey na wenzake wakimcheka.

"Huwezi kuwa unalala kwa mtu mwenye pesa. Itamuumiza mtu mmoja tu,” alihitimisha Rick Ross baada ya kumtania rafiki yake.

Hii hapa video hiyo;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved