Ninaweka pombe ili kumweka shetani mbali na nyumba yangu - Wajackoyah

“Ninaweka pombe ili kumweka shetani mbali na nyumba yangu,” Wajackoyah alisema.

Muhtasari

• “Ninaweka pombe ili kumweka shetani mbali na nyumba yangu,” Wajackoyah alisema.

WAJACKOYAH
WAJACKOYAH
Image: FACEBOOK

Wakili msomi na mwanasiasa George Wajackoyah amefichua sababu maalum ya kupenda kuweka pombe katika nyumba yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Wajackoyah alichapisha ujumbe huo ulionuia kuwajibu wale wanaohoji sababu ya yeye kuweka pombe kwa nyumba yake muda wote.

“Ninaweka pombe ili kumweka shetani mbali na nyumba yangu,” Wajackoyah alisema.

Mwanasiasa huyo mtata anajulikana na wengi kutokana na manifesto yake ya uchaguzi wa 2022 alipokuwa akiwania urais kupitia chama chake cha Roots.

Wajackoyah alikuwa anapigia debe uhalalishwaji wa bangi lakini pia Kenya kuanza kuuza nyama ya nyoka na mbwa kwa Wachina.

Hata hivyo, hakuweza kushinda uchaguzi huo baada ya kumaliza katika nafasi ya 3 na kura zisizozidi 60k.

William Ruto alishinda uchaguzi huo kwa kura zaidi ya milioni 7 huku Raila Odinga akiibuka wa pili na milioni 6 na ushee.

Chama cha Roots kilisambaratika siku chache baadae, kufuatia mvutano baina ya Wajackoyah na aliyekuwa naibu wake, Justina Wamae ambaye alimtuhumu kwa kuunga mkono Azimio chini ya maji na yeye akatishia kuunga mkono UDA.