logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nuru Okanga afukuzwa shule kwa kutongoza mwalimu mwaka 1 baada ya kuingia Form 1

Alisema kwamba kosa lililompelekea kufukuzwa ni tamaa ya macho kujaribu kumtongoza mwalimu wa kike.

image
na Davis Ojiambo

Burudani20 August 2024 - 09:51

Muhtasari


  • • Akizungumza kwenye chaneli ya Obinna, Okanga alifichua kwamba masomo yake yaligonga mwamba baada ya kufanya kosa lililompelekea kufukuzwa shuleni.
NURU OKANGA

Mwanasiasa Nuru Okanga amethibitisha kwamba haendelei na masono yake, mwaka mmoja baada ya kujiunga na shule ya upili kidato cha kwanza.

Akizungumza kwenye chaneli ya Obinna, Okanga alifichua kwamba masomo yake yaligonga mwamba baada ya kufanya kosa lililompelekea kufukuzwa shuleni.

Mtetezi huyo wa sera za kinara wa ODM, Raila Odinga alimwambia mbunge wa Kapseret Oscar Sudi kaitka kipindi hicho kwamba kwa sasa anajaribu kutafuta jinsi ya kunusuru ndoto yake ya kuendelea kimakosa baada ya kufukuzwa shule ya awali.

Alisema kwamba kosa lililompelekea kufukuzwa ni tamaa ya macho kujaribu kumtongoza mwalimu wa kike.

“Sijasoma lakini niko kidato cha kwanza, na hiyo kidato cha kwanza nimekuwa na masaibu ya hapa na pale nikashtukia nimetongoza mwalimu nikafukuzwa. Ni ukweli, mimi siwezi danganya,” Okanga alisema.

“Wakati nilifanya mtihani wa KCPE nilitangaza na nilijiunga kidato cha kwanza nikatangaza na tena nimefukuzwa juu ya macho marefu ya kuvizia nimetupwa nje. Natafuta tena chaguo pahali nitaenda kujiweka ili masomo yangu yaendelee. Na hiyo tabia sasa sitakuwa nayo, nitaenda kuzingatia masomo juu niko na watoto na mke,” aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved