Remcy Don, Mkenya anayejitambulisha kama ‘pacha’ wa msanii nguli kutoka Kanada, Jason Derulo amewashauri Wakenya wenzao wanaojidai kuwa na mfanano na mastaa wengine.
Kupitia insta story yake, Remcy Don aliwataka Wakenya wenzake wanaohisi kuwa wanafanana mastaa wengine, iwe ndani au nje ya Kenya na Afrika, kwanza kuhakikisha kwamba kuna mfanano wa kweli na wala si kukurupuka.
Pia alishauri kwamba baada ya kugundua unafanana staa mkubwa, unstahili kulifuatilia suala hio kwa utaratibu na upekee weney uhalisia na wala si kuhisi kwamba ni jukumu la staa huyo kukusaidia.
“Wakenya wenzangu, ni muhimu kulifuatilia suala la kuwa na mfanano wa celeb Fulani na umakini wenye uhalisia na heshima. Kma utakwenda kudai kufanana celeb Fulani, hakikisha una vigezo vinavyoweza kuonekana na mafanikio yanayoendana na hali zao. Sio tu mfanano wa nje bali ni kuhusu pia kuvaa muonekano wa staa huyo kimaisha,” Don alitema madini.
“Kujidai kuwa unafanana celeb Fulani wakati hauna mafanikio yoyote yanayoendana naye kutazima kabisa madai yako na hivyo kutufanya sisi wengine kuonekana kama mzaha. Hebu na tulenge kuwa wawakilishi wao na kuwa na heshima kwa maceleb ambao tunavutiwa nao,” Don aliongeza.
Kauli yake inajiri saa chache baada ya Wakenya kumshambulia kijana anayejidai kuwa anafanana mbunge Phelix Jalang’oo akidai kuwa mbunge huyo hamsaidii licha ya kumfanana.
Wakenya walimsuta kwa kauli hizo, wakisema kwamba kufanana na mtu maarufu si kigezo cha kumdai kukusaidia moja kwa moja.