Jalang’o amshauri Bradley Mtall kutumia vizuri fursa anazopata kutokana na umaarufu wake

“Ninatamani angeelewa jinsi brand yake ni kubwa kwa sasa, aitumie kutengeneza chapaa, mtu akimletea kitu sasa hivi achukue kwa sababu itafika wakati watu watamuona kama mtu wa kawaida tu," Jalang'o alisema.

Muhtasari

• Aidha, mbunge huyo alimsauri Bradley kukubali na kuchukua kila dili analowekewa mezani sasa hivi wakati jina lake liko kileleni.

JALANG'O AMSHAURI BRADLEY MTALL.
JALANG'O AMSHAURI BRADLEY MTALL.
Image: HISANI

Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor maarufu Jalang’o amemshauri Bradley Mtall kutumia vizuri fursa zote anazopata wakati huuu maarufu wake upo katika kilele.

Akizungumza kwenye podiksti ya Iko N ini na Mwafreeka, Jalang’o alisema kwamba ni vizuri Bradley kuwa makini na dili anazotia mkataba wa kibiashara nazo ili kuhakikisha atanufaika kwa muda mrefu baada ya umaarufu kupungua.

Mbunge huyo alisema kwamba umaarufu wa mtu huisha na kutokomea kama moshi kwa haraka sana Kenya, hivyo ni vizuri mtu anapopata fursa na kujihusisha na brand mbalimbali kutumia fursa hiyo kwa njia faafu.

“Sasa hivi tuna huyu jamaa mrefu, Bradley, Gen Z Goliath. Huyu ni mtu ambaye alikuwa na maisha yake ya kawaida, na wakati wa Mungu ukampambazukia anatambulika wakati wa maandamano ya Gen Z. na sasa hivi ako na hizi brand zote ambazo zinamtafuta, tunavyozungumza yuko Diani, mara yake ya kwanza kuabiri ndege ni jambo kubwa sana kwake na tunafurahia kwa ajili yake. Ame’endorse vitu vingi na mimi ninatumai kwamba watu wanaosimamia brand yake wataangalia vitu ambavyo vitamnufaisha kwa muda mrefu kuliko yeye tu kuwa mrefu,” Jalang’o alisema.

“Na hawa watu ambao wanaitumia brand yake sasa hivi natumai wanampa mikataba ya maana ambayo itamnufaisha kwa muda mrefu. Hatungependa kumuona Bradley amerudi tena katika maisha ya awali kama kamagera,” Jalang’o aliongeza.

Aidha, mbunge huyo alimsauri Bradley kukubali na kuchukua kila dili analowekewa mezani sasa hivi wakati jina lake liko kileleni.

“Ninatamani angeelewa jinsi brand yake ni kubwa kwa sasa, aitumie kutengeneza chapaa, mtu akimletea kitu sasa hivi achukue kwa sababu watu watazoea huo urefu wake kadri siku zinavyozidi kuenda na itafika wakati anaonekana mtu wa kawaida tu,” alisema.