Mwanashoshalaiti Huddah Monroe ameshauri kuwa akili timamu ndio kila kitu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanashoshalaiti huyo
amekiri kuwa aliamua kuwacha kutumia bangi
na tangu wakati huo, amekuwa na akili timamu.
Huddah ameongeza kusema kuwa aliamua kupunguza kiwango cha
mtindi alichokuwa akitumia na siku hizi huwa hakunywi sana.
“Niliamua kuwacha kuvuta bangi, siku hizi huwa sinywi sana. Na wacha
nikwambie, akili timamu ni kila kitu.”
Aliandika Huddah kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mapema mwaka huu kwenye mtandao wa IG, mwanashoshalaiti huyo
alisema kuwa uraibu wa pombe ndio janga kubwa linaloikumba taifa la Kenya na
bara la Afrika kwa ujumla.
Wakati huo aliaema kuwa alifanya uchunguzi na kubaini kuwa
kila wakati alikuwa anakunywa pombe ilikuwa inamfanya kuwa na hasira, kichwa
ngumu na kuwa na machungu mengi mno.
Aidha Huddah amesema kuwa amewacha kuvuta bangi licha ya
awali mwaka huu kusema kuwa ni afadhali kuvuta bangi badala ya kunywa pombe.
“Nikakunywa siku hizi kusherehekea sio kulewa na
kuharibu mambo…Ninakuwa mtu mwingine. Hasira, uchungu na mkorofi. Kila kitu
kinaniudhi nikiwa mlevi.”
Alisema Huddah mwezi wa Juni kupitia IG yake.