
Mtengenezaji wa maudhui ya mtandaoni Mjaka Mfine ameomba radhi kwa wafuasi wake baada ya video aliyofanya ya challenge ya wimbo unaotambaa mtandaoni mapangale na Crazy Kennar kusambaa mtandaoni.
Baadhi ya wakenya mtandaoni wamekashifu kushiriki kwake katika challenge hiyo, wakidai kuwa kushiriki kwake ni sawa na kuunga mkono visa vya mauaji ya wanawake ambavyo vimekithiri nchini katika muda wa miezi mitatu iliyopita.
Aidha katika video aliyochapisha kwenye akaunti yake ya tik tok, Mjaka Mfine ameelezea kuomba radhi kwa wafuasi wake walioonekana kukwera naye kufanya challenge hiyo.
“Niko hapa kuomba msamaha… juzi nimefanya video na Crazy Kennar ya mapangale. Nilifanya challenge hiyo kwa sababu niliona ikiwa challenge sikuwa najua itashika watu wengi.” Alisema Mjaka Mfine
Kwa mujibu wake, Mjaka Mfine amesema kuwa alikuwa baadhi ya wanawake wa kwanza kabisa kuunda video ya kukashifu visa vya mauaji ya wanawake kupitia kaziyake ya kutengeneza maudhui.
“Hivi maajuzi nilitengeneza video kuhusu mauaji ya wanawake, nilikuwa mmoja wa watengenezaji maudhui wa kwanza kuongelelea jinsi wanwake wanauliwa tukitaka visa hivyo kusitishwa.” Aliongeza kusema Mjaka Mfine.
Mjaka Mfine ameomba msamaha kwa wafuasi ambao alisema kuwa alisoma jumbe zao kwenye mtandao wake wa kijamii waliokashifu kuhusika kwake kwenye challenge ya mapangale.
Mjaka Mfine amesisitiza kuwa hakufanya challenge hiyo kwa
malengo ya kuunga mkono mauaji ya wanawake. Vile vile amesema kuwa amefuta video
za challenge hizo alizochapisha mtandaoni akisema kuwa ameelewa alichokifanya.
