Msanii wa Afrobeat David Adedeji Adeleke maarufu kama Davido amesafirisha magari yake mapya mawili aina ya Tesla Cyber Truck na Rolls Royce Spectre kutumia ndege hadi nchi alikozaliwa Nigeria.
Msanii huyo amekuwa msanii wa muziki wa kwnza barani Afrika kununua gari aian la Tesla Cyber Truck linalotengenezwa na kampuni inayomilikiwa na Elon Musk ambaye hivi maajuzi aliteuliwa na rais mteule wa Marekani kwenye serikali yake.
Davido alichapisha picha na video za magari yake hayo mawili yakipakiwa kwenye ndege ya mizigo iliyokuwa ikielekea nchini Nigeria.
Gari aina la Tesla Cyber Truck ambalo Davido amenunua linakisiwa kumgharimu dola 165,000 za Marekani sawia na takribani shilingi milioni 21 za Kenya huku Rolls Royce Spectre ikigharimu dola 544,000 sawia na shilingi takribani milioni 70. Hata hivyo ada ya kusafirisha magari hayo kwenye ndege haijawekwa wazi na msanii huyo.
Msanii yupo nchini Uholanzi na anatarajiwa kufanyiwa mahojiano
na chombo kimoja cha habari cha jijini Amsterdam, Uholanzi manmo Ijumaa kabla
ya kutumbuiza mashabiki wake siku ya Jumamosi tarehe 30 Novemba kwenye burudani
la Ziggo Dome.