logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hali ya mwimbaji Jose Chameleone yafichuliwa baada ya kukimbizwa hospitalini akiwa mgonjwa mahututi

Iliripotiwa kuwa alikuwa amekimbizwa hospitalini baada ya kuugua sana.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako13 December 2024 - 07:27

Muhtasari


  •  Usimamizi wa Chameleone, katika taarifa ulithibitisha kwamba msanii huyo mwenye kipaji aliugua na alikuwa amelazwa hospitalini.
  • Mwaka jana alikuwa amelazwa hospitalini nchini Marekani ambako alifanyiwa upasuaji kufuatia matatizo ya tumbo.


Mnamo siku ya Alhamisi, Desemba 12, mwimbaji maarufu wa Uganda Joseph Mayanja almaarufu Jose Chameleone aliripotiwa kuwa mgonjwa mahututi.

Video za kutisha za mwimbaji huyo mkongwe akikimbizwa hospitalini kwa gari na kubebwa hadi wodini kwa machela zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua wasiwasi kutoka kwa mashabiki wake na wapenzi wa muziki. Iliripotiwa kuwa alikuwa amekimbizwa hospitalini baada ya kuugua sana.

Baadaye jioni, usimamizi wa Chameleone, katika taarifa ulithibitisha kwamba msanii huyo mwenye kipaji aliugua na alikuwa amelazwa hospitalini.

“Kwa mashabiki na wapenzi wote wa Leone Island Music Empire, tunaelewa kuwa habari za kulazwa hospitalini kwa Jose Chameleone zinaweza kuwa zimesababisha wasiwasi na wasiwasi. Tunataka kuwahakikishia kuwa Chameleone anapokea matibabu na uangalizi bora zaidi, na tuna matumaini kuhusu kupona kwake,” taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Facebook wa Chameleone ilisoma.

"Tunashukuru kumiminika kwa upendo, usaidizi, na maombi kutoka kwa mashabiki na wasanii wenzetu. Ujumbe wenu una maana kubwa kwa Chameleone na familia yake wakati huu,” wasimamizi walisema zaidi.

Uongozi wa mwimbaji huyo pia uliomba sapoti na faragha kwa familia yake anapoendelea na matibabu.

“Tunakuomba uheshimu faragha ya Chameleone na ya familia yake wanapopitia kipindi hiki kigumu. Tutawafahamisha kuhusu hali yake na tunathamini usaidizi wenu unaoendelea na maombi,” alisema.

“Tujumuike pamoja kutuma upendo, mihemko chanya, na maombi kwa mpendwa wetu Chameleone. Tuna imani kwamba atarejea kwa nguvu zaidi na kuendelea kutuburudisha na kututia moyo kwa muziki wake. #Get WellChameleone #PrayersForChameleone," taarifa hiyo ilisema.

Chameleone ni mmoja wa wanamuziki nguli wa Uganda ambaye amekuwa akiburudisha ukanda wa Afrika Mashariki kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Si mara ya kwanza anaripotiwa kuwa mgonjwa mahututi. Mwaka jana alikuwa amelazwa hospitalini nchini Marekani ambako alifanyiwa upasuaji kufuatia matatizo ya tumbo.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved