Mtengenezaji wa maudhui ya mtandaoni Terence Creative amewashauri wanandoa kuvumiliana wakati mmoja wao yupo chini kimfuko badala ya kuweka wazi masaibu wanayopitia kwenye ndoa zao.
Kwa mujibu wa Terence, haoni tatizo ikiwa mpenzi wa kiume anaweza ‘kuwekwa’ na mpenzi wake wa kike haswa wakati anapitia changamoto za kukosa kuwajibikia mahitaji ya familia kwa kukosa pesa wakati mchumba wake ana uwezo wa kukimu mahitaji ya kinyumbani ama ya kimapenzi.
Mtengenezaji huyo wa maugdhui aidha amewataka wanawake kuwasaidia wanaume wao kwenye ndoa hadi wakati ambapo watafanikiwa kuwa na pesa na kuendelea kukidhi mahitaji yao.
“Hakuna shida mwanamume kuwekwa na mwanamke, wanawake ikiwa mume wako hayuko vizuri kihela, mpe sapoti na umheshimu.” Alisema Terence.
Hata hivyo, Terence amewarai wanawake walio na uwezo wa kihela na ambao waume zao wamekosa kukimu mahitaji ya nyumbani kuwapa pesa ili watekeleze majukumu yao kama vichwa vya familia akiwakata kuwacha kuwaanika mbele ya umma.
Terence ambaye amekuwa kwenye mahusiano na mkewe Milly Cheby kwa Zaidi ya miaka 11, ametumioa mfano wao akisema kwamba kuna wakati aikuwa amewekwa na mke wake kwa zaidi ya miaka 4. Terence amesema kwamba mkewe alikuwa anawajibikia takribani asilimia 98.9 ya bili zote.
“Mimi niliwekwa kwa Zaidi ya miaka 4 na Milly Chebby wakati huo nikiwa namchumbia na sasa ni mke wangu wa miaka 11, alikuwa analipa asilimia 98.9 ya bili.” Aliongeza kusema Terence.
Mchekeshaji huyo hata hivyo amewataka wanaume kujituma katikajuhudi zao huku akiwataka wanawake kuacha kuanika waume zao na badala yake kuwavumilia akiwashauri kwamba upo wakati watafanikiwa na watawaweka pia.