Mwimbaji wa nyimbo za injili na za mapenzi Moses Tarus Omondi almaarufu Mr Seed hivi majuzi alitembelea kaburi la marehemu mamake alipokuwa kijijini kwao katika Kaunti ya Siaya.
Msanii huyo alichapisha video yake akiwa amezama katika hisia kali mahali alikozikwa mamake huku akifuta vumbi juu ya kaburi hilo.
Chini ya video hiyo aliyoichapisha kwenye Instagram, alikariri mapenzi yake kwa mamake na kuitakia roho yake iendelee kupumzika kwa amani.
“Nakupenda mama, endelea kupumzika maah! Bado ninaendelea kusukuma mbele,” Mr Seed aliandika.
Haya yanajiri takriban miezi minne baada ya mamake mwimbaji huyo, Bi Teresa Auma Otieno kuzikwa nyumbani kwake Siaya mnamo Septemba 14, 2024.
Mr Seed alitangaza kifo cha mamake mpendwa mwishoni mwa Agosti mwaka jana, siku chache baada ya kuwaomba mashabiki wamwombee.
Mwimbaji huyo alitumia mitandao yake ya kijamii kutangaza kifo chake katika ujumbe mfupi uliosomeka;
"Pumzika sasa mpenzi wangu ���� nitakupenda milele ����." Aliandika
Katika ujumbe wa hisia wa hapo awali, mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi alisema mamake alikuwa amelazwa na kutoka hospitalini mara kadhaa.
"Nimekuwa nikiingia na kutoka katika hospitali mbalimbali kwa muda wa mwaka 1 na nusu nikijaribu kutafutia mama yangu matibabu.. inasikitisha sana kuona mama yetu akiteseka kila siku ���� .. lakini bado Mungu ni mwaminifu na tunamtumaini na kumuombea apone. .. kwa sasa amelazwa @thelutonhospital wanamhudumia vyema, wauguzi na madaktari wote wanaofanya kazi usiku na mchana Mungu awabariki sana ."
Aliwashukuru madaktari waliokuwa wakimhudumia mama yake.
“Shukrani za kipekee kwa @lasante_paramedics kwa kutoa gari lao la wagonjwa tukaenda mpaka Eldoret kwenda kumchukua na kumrudisha ���� Jamani tusaidieni kwenye maombi..hali yake sio nzuri ila tunamuombea apone,” aliandika.